Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, February 6, 2015

PICHA ZA MATUKIO KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Februari 6, 2015. Kutoka kushoto ni Yahya Kassim Issa wa Chwaka, Jerome Damas Bwanausi wa Lulindi, Muhammad Amour Chombo wa Magomeni na Mussa Hassan Mussa wa Aman.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wabunge kwenye jengo la utawala la Bunge mjini Dodoma Februari 6, 2015. Kutoka kushoto ni Yahya Kassim Issa wa Chwaka, Jerome Damas Bwanausi wa Lulindi na Muhammad Amour Chombo wa Magomeni .
Mbunge wa Vunjo na Mwenyekiti wa TLP akiteta na Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCC MAGEUZI,James Mbatia (kushoto) bungeni mjini Dodoma Februari 6,2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)



Mwenyekiti wa kamati teule ya Bunge iliyokuwa inashughulikia matatizo ya Ardhi hapa Nchini Mhe. Christopher Ole Sendeka akiwasilisha Ripoti ya kamati yake katika kikao cha Bunge mjini Dodoma mapema leo.
Wadau wa Ardhi Kutoka jamii ya wafugaji na wakulima wakiwa wamekaa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakifuatilia wakati Mwenyekiti wa kamati teule ya Bunge iliyokuwa inashughulikia matatizo ya Ardhi hapa Nchini,  Mhe. Christopher Ole Sendeka akiwasilisha Ripoti ya kamati yake katika kikao cha Bunge mapema leo. 
Watumishi wa kampuni ya Masu Entertrade wakiwa wabebeba makabrasha yenye ripoti ya kamati teule ya Bunge iliyokuwa inashughulikia migogoro ya Ardhi hapa nchini wakiwa wanaelekea ndani ya ukumbi wa Bunge.Picha na Deusdedit Moshi Globu ya Jamii Kanda ya Kati.

No comments:

Post a Comment