Beki wa Manchester United Chris Smalling ni moja kati ya
wachezaji ambao wamekuwa wakilaumiwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na
ubovu wa safu ya ulinzi ya United ambayo imekuwa ikiruhusu sana mabao kufungwa
.
Ni vigumu kuamini kuwa beki huyu ambaye alijiunga na United
miaka minne iliyopita leo hii ndiyo mchezaji mwenye kasi kuliko wote kwa mujibu
wa takwimu za klabu hiyo .
Chris Smalling ndio mchezaji mwneye kasi kuliko wote ndani
ya Man United.
Hii ni siri iliyofichuliwa na mshambuliaji wa Manchester
United James Wilson ambaye salisema kuwa kuna wachezaji wengi wenye kasi kwenye
timu hiyo lakini hakuna anayemzidi Chris Smalling.
Wilson amezungumza haya kwenye mahojiano maalum ambapo
alisema kuwa wanapokuwa uwanjani huwa wanavalishwa vifaa maalum vya GPS ambavyo
kwa msaada wa teknolojia ya kisasa humsaidia kocha na wasaidizi wake kutambua
jinsi wachezaji wanavyofanya mazoezi pamoja na kasi waliyo nayo na umbali ambao
wanakimbia .
Kwa mujibu wa takwimu zilizokusanywa na kifaa hicho hakuna
mwenye kasi kama Chris Smalling ndani ya kikosi cha Man United .
James Wilson pia amewataja wachezaji wengine kama Ashley
Young , Luke Shaw Antonio Valencia pamoja na yeye mwenyewe kama wachezaji
wengine wenye kasi lakini bado hakuna anayemzidi Smalling.
No comments:
Post a Comment