Seneta mmoja nchini Marekani amewataka wamiliki wa migahawa
nchini humo kuacha tabia ya kuwashurtisha wafanyakazi wao kunawa mikono baada
ya kutoka maliwatoni.
Seneta Thom Tillis, wa chama cha Republican kutoka North
Carolina ,ametoa kauli hiyo mapema wiki hii wakati alipokuwa akipinga kanuni za
biashara na kuwataka wafanyakazi waachwe waamue wenyewe kuosha mikono yao, ama
lah.
Kauli ya seneta huyo imekuja baada ya kanuni kuelekeza kuwa
mgahwa ambao hautawaelekeza
wafanyakazi wake kunawa mikono,waache kufanya
biashara haraka.
Seneta Tills, akashauri kuwa migahawa ambayo wafanyakazi
wake hawanawi mikono wanapaswa kuweka alama wazi kwa wateja wao kama ishara ya
utaratibu wao,kauli hii ya pili Tillis aliitoa wakati wa mahojiano na Us
Capitol.
Tills akatetea hoja yake kwamba, Kuna wakati zipo kanuni
ambazo pengine tunahitaji kuzipa muelekeo,lakini waachi wale ambao wamewekewa
kanuni hizo hiyo waamue kama ina leta maana ama lah na wafanye maamuzi hayo
kinyume na serikali.
Hoja hii imekuja huku wagombea uraisi walio wengi kutoka
katika chama cha Republican,wakiamini kwamba wataulizwa maswali kuhusiana na
kanuni na taratibu za chanjo ya ugonjwa hatari wa Ebola
Walau wazazi wawili wao wameonesha msimamo wa dhahiri kuwa
wakati mwingine huwataka watoto wao kuikwepa chanjo hiyo pindi wanapohudhuria
masomo yao.
No comments:
Post a Comment