Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, February 24, 2015

PICHA 18: MEZ B AZIKWA MAKABURI YA WAHANGA MJINI DODOMA



 Baadhi ya wasanii wa Muzik wa Kizazi kipya wakiwa wamebeba Sanduku lililokuwa na Mwili wa aliyekuwa Msani wa muziki huo maarufu kama Bongo Fleva Marehemu  Mez B wakati wakiwasili katika viwanja vya mashujaa mjini Dodoma kwa ajili ya kuuagwa. (Picha na John Banda wa Pamoja Blog)


Maelfu ya watu wa mji wa Dodoma wamejitokeza kuaga mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya marehemu Mez B viwanja vya Mashujaa jana mchana mjini Dodoma.
Baada ya kuagwa mwili wa marehemu Mez B, mwili huo ulipelekwa  kwenye makaburi ya Wahanga yaliyopo eneo la Maili Mbili mjini Dodoma na kufanyiwa ibada yamazishi.
Wasanii wa kundi la la Chemba Squad, Nurah na  Dak Master wakisoma historia ya Marehemu Mez B alipoanzia Kimuziki kabla ya kuuaga mwili wake kwa ajili ya mazishi yaliyofanyika Mailimbili kwa wahanga wa treni.





Bw. Tumsifu Mwasamale akisoma hotuba fupi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakati wa kuagwa kwa mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya pia alikuwa anawakilisha kundi la la Chemba Squad.
 Mama Mzazi wa Marehemu Marry Mkandawile akiuaga Mwili wa Marehemu Moses Maarufu kama Mez B katika viwanja vya Mashujaa mjini Dodoma kabla ya mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya wahanga wa Treni Maili mbili, aliyemshikilia mama  ni mmoja wa wanamuziki wa kundi la chemba Squad Nurah kundi ambalo marehemu alikuwa mshiriki
 Baba Mdogo wa Marehemu Mez B akiuaga Mwili huo
 Maelfu ya wakazi wa mji wa Dodoma wakiwa katika viwanja vya Mashujaa walipokuwa wakiuaga mwili wa Marehemu Mez B.

Picha na John Banda wa Pamoja Blog


Pichani ni Mama mzazi wa Mez B akiwa ameshikiliwa na ndugu baada ya kuingia viwanja vya Mashujaa ili kutoa heshima za mwisho. Marehemu Mez B baada ya kuagwa na mashabiki wa mziki pamoja na ndugu jamaa na marafiki mwili wake ulielekea kupumzishwa katika makaburi ya Wahanga Maili mbili.
Mungu ailaze roho ya marehemu Mez B mahali pema peponi
Amin
IMG-20150223-WA0037 IMG-20150223-WA0038
Baadhi ya wasanii waliohudhuria msiba huu wa Mez B wakiwa kwenye majonzi mazito
IMG-20150223-WA0039 IMG-20150223-WA0040 IMG-20150223-WA0041 IMG-20150223-WA0042 IMG-20150223-WA0044
Mtangazi wa Citizen TV anayejulikana kwa jina la Mzazi Willy Tuva akifanya mahojiano na msanii wa Bongo Fleva Janjaro.

No comments:

Post a Comment