Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, April 10, 2015

POLISI WAKANUSHA TISHIO LA MAGAIDI KUSHAMBULIA CHUO CHA UHASIBU ARUSHA



KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas,  amekanusha uvumi ulioenea katika mitandao ya jamii kuhusu kukamatwa magaidi  mkoani  Arusha usiku wa kuamkia leo waliokuwa wamejitayarisha kukishambulia Chuo cha Uhasibu (Institute of Accountancy Arusha - IAA) wakidaiwa kuwa na gari 
 
aina ya Toyota Premio nyeusi ikiwa na watu wanne na bunduki nne aina ya SMG na risasi 160 walipojaribu kuingia chuoni hapo.

Inadaiwa katika taaifa hiyo isiyojulikana chanzo chake kwamba watu hao walijifanya  ndugu wa mwanafunzi mmoja wa kike anayeishi kwenye hosteli zilizo ndani ya chuo hicho.

Rais wa chuo hicho, Iman Mkumbo, naye  amesema  habari hizo hazina ukweli wowote.

No comments:

Post a Comment