Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, April 8, 2015

Wakazi wa Nkololo Bariadi mkoani Simiyu walalamikia kukosa umeme miezi miwili mfululizo.


Wakazi wa kata ya Nkololo bariadi mkoani Simiyu wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa umeme kwa zaidi ya miezi miwili tangu ulipokatika mwezi wa pili na kusababisha kupanda kwa ghalama za maisha na kuongezeka kwa matukio ya wizi na uvunjaji wa nyumba unaotokana uwepo wa giza huku wakishangaa shirika ya umeme (Tanesco) na wakala wa umeme vijijini (REA) wakiendelea kutupiana mpira kana kwamba wote hawa husiki na suala ilo bila kujali madhara wanayo yapata wananchi.
Wakizungumza na ITV iliyotembelea katika eneo ilo 

 
wakazi wa Nkololo wamesema tangu umeme ulipo katika mwezi wa pili mwaka huu hadi sasa hawajapatiwa ufumbuzi na wanapo piga simu Tanesco hakuna jibu wanalo pata huku wananchi wakiendelea kuteseka kwa kukosa huduma hiyo muhimu.
Kwa upende wao baadhi ya viongozi wa halmashauri ya Bariadi wamesema hali hiyo imesababisha kuongezeka kwa matukio ya wizi ujambazi na uvunjaji wa maduka yanayo tokana na uwepo wa giza nene nyakati za usiku na wamekuwa na wakati mgumu katika uongozi wao sasa wanatarajia kupeleka kero katika baraza la madiwani.
Diwani wa kata ya Nkololo Masunguro Mbushi amesema ameshapeleka kero hiyo kwa uongozi wa shirika la ugavi wa umeme Tanesco na kuahidiwa kuwa litamalizika baada ya wiki mbili lakini hakuna dalili na ajabu zaidi watu wanaendelea kukatwa fedha za huduma ya umeme bila huruma.
ITV ilifika katika ofisi ya shirika la Tanesco wilaya Bariadi kumwona meneja Bwana Geogle Madaha ili kupata ufafanuzi wa kero hiyo bila mafaniko baada ya ofisi kuwa zimefungwa kwa mapumziko marefu ya sikuku ya pasaka na siku ya karume na tulipo mpigia kwa simu yake ya mkononi alisema yupo mbali na ofisini lakini juhudui za kumtafuta zinaendelea.(ITV)

No comments:

Post a Comment