Picha kutoka Maktaba
Kufuatia watu wawili waliojeruhiwa na watu waliokuwa wamejigunika nyuso zao huko katika mtaa wa Makunduchi Zanzibar waliokuwa wakienda kujiandikisha katika daftari la wapiga kura, mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Mhe Prof.Ibrahimu Lipumba ametoa tamko la kulaani kitendo hicho.
Akiwahutubia wananchi katika viwanja vya sabasaba wilayani Buhigwe mkoani kigoma mwenyekiti huyo Mhe.Lipumba amesema kitendo hicho si cha kuvunilia.
Aidha Mhe.Lipumba amemtaka rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kama amiri jeshi mkuu kuhakikisha amani na usalama vinaendelea kuwepo wakati tukielekea katika uchaguzi mkuu ujao.
No comments:
Post a Comment