Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, July 24, 2015

Tazama Picha za utotoni za Mario Balotelli, Messi, Kaka

1. Lionel Messi
lionel-messi-barcelona-la-liga3248555-1425893997-2343424
Lionel Messi
Alizaliwa Juni 24 1987 Rosario Argentina baba yake Jorge Horacio Messi alikuwa mfanyakazi katika kiwanda cha chuma Argentina na mama yake Celia María Cuccittini alikuwa msafishaji.
Akiwa na umri wa miaka mitano Messi alianza kucheza soka katika klabu ya Grandoli ya mtaani kwao ambapo kocha wa timu hiyo alikuwa baba yake.
messi 1
Lionel Messi
Mwaka 1995 Messi alijiunga katika timu ya vijana ya Newell’s Old Boys ambayo ndani ya miaka minne ilipoteza mechi moja pekee, akiwa na umri wa miaka 11 Messi alipata matatizo ya ukuaji, ugonjwa ambao ulikuwa unagharimu matibabu dola 900 kwa mwezi ambayo ni zaidi ya Tsh 1900,000/= kiasi ambacho klabu na familia yake hawakuwa na uwezo wa kugharamia.
6296667_orig
Lionel Messi wakati alipokuwa mdogo
Mkurugenzi wa michezo wa FC Barcelona wakati huo Carles Rexach akakubali kukiokoa kipaji cha Messi na kumchukua Messi pamoja na baba yake ili 

akamuangalie Messi wakati anapatiwa matibabu Barcelona alijiunga La Masia kituo cha kukuzia vipaji vya soka kinachomilikiwa FC Barcelona.
9128763_orig
Lionel Messi wakati alipokuwa mdogo
2. Ricardo Kaka
pic_1297024839_8
Ricardo Kaka
Ricardo Kaka hakuwa tofauti sana na vijana au watoto wengi wa Afrika ambao huwa na tabia ya kujifunza vitu tofauti tofauti wakati wakiwa wadogo, licha ya kuwa hakutokea katika familia yenye maisha magumu, kipindi ana umri wa miaka 8 aliwahi kucheza tennis kabla ya kuamua kujikita katika soka.
kaka 1
Ricardo Kaka katika muonekano wake akiwa mdogo
Kaka baba yake alikuwa engeneer na mama yake alikuwa mwalimu kwa hiyo suala la fedha kwao haikuwa tatizo kitu kilichomfanya aweze kumudu kupata elimu na kucheza soka… Uwezo wake wa soka ulianza kuonekana akiwa na miaka 15 wakati ambao alikuwa akiichezea timu ya shule ya Alphaville ndipo klabu ya Sao Paulo ilipomuona na kumpa nafasi ya kujiunga katika Academy ya Sao Paulo.
kaka
Ricardo Kaka katika muonekano wake akiwa mdogo
Alipokuwa na umri wa miaka 18 Kaka alipata mkasa ambao huenda ungeweza msababishia kuachana na soka baada ya kupata ajali wakati akiwa anaogelea katika swimming pool na kusababisha tatizo katika uti wa mgongo kitu ambacho kingeweza kupelekea apate ugonjwa wa kupooza.
kaka (1)
Ricardo Kaka
3. Mario Balotelli
Balotelli-pic
Mario Balotelli
Jina lake kamili ni Mario Barwuah raia wa Italia, wazazi wake ni wahamiaji kutokea Ghana, wakati ana umri wa miaka mitatu wazazi wake walishindwa kumtunza na kumtoa katika familia ya kizungu ya Francesco Balotelli na mkewe Silvia wamlee hapo ndipo alipolipata jina lake la Balotelli.
ballotei
Mario Balotelli wakati alipokuwa mdogo
Balotelli aliwahi kuwalaumu wazazi wake wa kumzaa kuwa walimtelekeza licha ya kuambiwa kuwa hawakuwa na uwezo wa kumtunza, kazaliwa na kukulia Italia ila kutokana na asili ya wazazi wake Balotelli alikuwa na uwezo wa kuichezea timu ya taifa ya Ghana kabla ya mwaka 2008 kupewa uraia wa Italia na kutangaza kuwa yeye ni muitaliano.
ballotelli
Mario Balotelli wakati alipokuwa mdogo na ndugu zake
“Mimi ni muitalia, naipenda Italia na siku zote nitacheza timu ya taifa ya Italia”>>>Mario Balotelli
balotelli_3124312k
Mario Balotelli
Story Imeandaliwa na Millard Ayo

No comments:

Post a Comment