Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, September 29, 2015

FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU

FAHAMU UGONJWA WA BAWASIRI AU KUOTA KINYAMA SEHEMU YA HAJA KUBWA NA NAMNA YA KUEPUKA NA UGONJWA HUU(JAMIIMOJABLOG)
~watu wengi wanasumbuliwa na tatizo hili ambalo huwafanya kuwa na uoga na aibu wa kuelezea na kushindwa hata kwenda hospital kupata tiba
JE, UNAJUA BAWASIRI/HEMORRHOIDS NI NINI????!!
~Ni ugonjwa unaotokana na kuathirika kwa mishipa ya damu ya ndani na nnje ya sehemu ya haja kubwa na wakati mwingine mishipa hiyo huweza kupasuka/kuteleza na kuvuja damu kwenye njia ya haja kubwa na kasababisha kutoka kinyama au uvimbe
~ugonjwa huu wa bawasiri kwa lugha ya kitaalamu tunauita HEMORRHOIDS ilhali kwa lugha ya kingereza unafahamika kama piles
~tatizo hili huwaathiri watu wote ila zaidi huwaathiri watu wazima kuliko watoto na inakadiriwa kuwa karibu 50%ya watu wote wako katika hatari ya kupata tatizo hili katika umri wa miaka 30_50
AINA ZA BAWASIRI
~Kuna Aina mbili za bawasiri
(A) BAWASIRI YA NDANI
~Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa huwa haiambatani na maumivu na wengi huwa hawajitambui kuwa Wana tatizo hili
~Aina hii hutokana na kuvimba na kuharibika kwa mshipa wa artery za ndani ya mfereji wa haja kubwa
~Aina hii imegawanyika katika madaraja manne
(1)DARAJA LA KWANZA ~Hii ni bawasiri ambayo haitoki mahal pale panapohusika
(2)DARAJA LA PILI ~hii hutokea wakati wa haja na kurudi yenyew ndani baada ya kujisaidia
(3)DARAJA LA TATU :hii hutokea wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kurudisha ndani yeye mwenywe 

 
(4)DARAJA LA NNE :hii ni bawasiri inayotoka na huwa ngumu kurudi
(B)BAWASIRI YA NNJE
~Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa na huambatana na maumivu makali na kuwashwa kwa ngozi katika eneo la tundu Hilo pia husababisha mishipa ya damu (vena) kupasuka na damu kuganda na kasababisha Aina ya bawasiri iitwayo THROMBOSED HEMORRHOIDS
CHANZO CHA TATIZO
~chanzo halisi cha ugonjwa huu hakijapatikana ila Kuna vitu ambavyo huwa chanzo cha kupata ugonjwa wa bawasiri ambayo ni ÷
White right pointing backhand indexKUFANYA MAPENZI KINYUME NA MAUMBILE
White right pointing backhand indexKUHARISHA KWA MUDA MREFU
White right pointing backhand indexTATIZO LA KUTOPATA CHOO
White right pointing backhand indexMATATIZO YA UMRI
White right pointing backhand indexKUKAA KITAKO KWA MUDA MREFU
White right pointing backhand indexUZITO KUPITA KIASI
White right pointing backhand indexMATUMIZI YA VYOO VYA KUKAA KWA MUDA MREFU
DALILI ZA BAWASIRI
White right pointing backhand indexNgozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
White right pointing backhand indexkupata maumivu makali wakati wa kujisaidia
White right pointing backhand indexkutokea uvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
White right pointing backhand indexkujitokeza kwa kinyama katika eneo la tundu Hilo
White right pointing backhand indexkinyesi kuwa na damu na kunuka harufu mbaya sana
MATIBABU NA JINSI YA KUEPUKA TATIZO LA BAWASIRI
~matibabu ya bawasiri hutegemea na Aina ya bawasiri pia tiba iliyozoeleka ni kukatwa kinyama na kuendelea na lishe ya chakula hata hvyo tiba hii si nzuri kwasababu huwa haitibu chanzo cha tatizo hivyo huwa rahisi kujirudia hivyo tiba nzuri ni kutumia dawa na anion chip kubandika mahali penye tatizo na kuondoa tatizo Hilo
~Pamoja na hayo bawasiri ni ugonjwa unaoweza kuepukika kwa kuzingatia
White right pointing backhand indexKULA MBOGAMBOGA ZA MAJANI, MATUNDA, NA NAFAKA ZSZOKOBOLEWA
White right pointing backhand indexKUNYWA MAJI MENGI ANGALAU GRASS 6/12 Kwa siku
White right pointing backhand indexEPUKA KUKAA CHOONI KWA MUDA MREFU
MADHARA YA TATIZO LA BAWASIRI
White right pointing backhand indexkupata upungufu wa damu (anemia)
White right pointing backhand indexKupata tatizo la kutokuweza kuhimil choo
White right pointing backhand indexhupunguza nguvu za kiume na kuondoa hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake
White right pointing backhand indexkuathirika kisaikolojia
White right pointing backhand indexkukosa moral ya kufanya Kaz kutokana na maumivu makali
WASILIANA KWA 0717035770 AU 0753692612.

No comments:

Post a Comment