Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, September 25, 2015

SIRI IMEFICHUKA: ZENGWE MILION 6 ZA KAJALA KWA TIFFAH

Musa Mateja
Imevuja! Yale mamilioni ya staa wa sinema za Kibongo, Kajala Masanja ‘Kay’ aliyommwagia mwandani wa msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kama zawadi ya mwanaye, Latiffah Nasibu ‘Princes Tiffah’ yamepigwa zengwe.


Awali, habari zilizolifikia gazeti ndugu la hili, Risasi Mchanganyiko la Jumatano iliyopita zilieleza kwamba, Kajala alitumia takriban dakika ishirini kummwagia Zari ‘minoti’ ya elfu kumikumi kwenye pati ya arobaini ya Tiffah iliyofanyika nyumbani kwa Diamond, Madale-Tegeta jijini Dar, Jumapili iliyopita.


Katika maelezo yake kwenye habari hiyo, Kajala alisema kuwa alimtunza Zari kama waalikwa wengine walivyofanya bila kujali watu watasema nini.

Kwa mujibu wa Kajala, manoti hayo yalikuwa takriban shilingi milioni sita za madafu, jambo lililoibua maswali ikidaiwa kwamba, si kweli hakikuwa kiasi hicho na badala yake, mwigizaji huyo alitaka kujipaisha.
“Hata ukiangalia video za tukio hilo, utaona Zari alikuwa akicheza kitu kama Kibao-Kata wakati Kajala akichomoa ‘misimbazi’ kwenye waleti na kumtupia mama Tiffah.

“Ukweli ni kwamba hata waleti yenyewe ilikuwa nyembamba kiasi kwamba ingekuwa na kiasi hicho ingeonekana imevimba.
“Kilichotokea ni kwamba ile video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii ilikuwa inajirudiarudia na kuwafanya watu kuona kama Kajala alitoa noti nyingi kiasi hicho.

“Ukweli ni kwamba hata shilingi milioni mbili hazikufika. Si unajua tena Wabongo kwa kujipaisha? Habari ndiyo hiyo,” kilidai chanzo chetu na kuongeza:

Wakati mamilioni ya Kajala yakipigwa zengwe, kwa upande wake, mwigizaji mwingine wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel Grayson ambaye naye alidaiwa kumfanyia kufuru ya kummwagia Zari noti, naye ameibuka na kudai kwamba, yeye alitunza kiasi cha shilingi milioni tano ambazo nazo ziliibua maswali.
“Mimi nilimtunza Tiffah kama shilingi milioni tano hivi, kama kuna mtu mwenye swali atajijua mwenyewe kimpango wake,” alifunguka Aunt kwa kifupi.

No comments:

Post a Comment