Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, September 25, 2015

WEMA SEPETU AMLIZA MAMA YAKE SHARO MILIONEA

Mama wa msanii marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’ akilia.
Wasanii mbalimbali wa filamu waliomo kwenye Kampeni za CCM kupitia mpango wa Mama Ongea na Mwanao akiwemo Wema Sepetu, juzikati walimliza mama wa msanii marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’ pale walipokwenda kutembelea kaburi lake.
Wema Sepetu akifuta machozi.
Wasanii hao walichukua uamuzi huo walipopita katika kijiji alichozaliwa msanii huyo cha Lusanga, wilayani Muheza mkoani Tanga na kwenda kumsalimia mama wa marehemu lakini ilidaiwa kuwa Wema alimliza mama huyo baada ya kuonekana akilia sana bila kunyamaza.Aliyekuwa msanii wa bongo fleva, marehemu Hussein Mkiety ‘Sharo Milionea’
“Tulipofika pale tulionana na mama Sharo, tukapiga naye stori mbili tatu lakini tuliona tusiishie pale, tupelekwe kwenye kaburi la mwanaye, hapo ndipo alipoanza kubadilika na kuonesha hali ya majonzi kisha akaanza kulia!
“Hali ile ilitufanya wote tuliokuwa pale kupatwa na huzuni na kwa kweli wengi tulishindwa kujizuia kulia, hata tulipofika kaburini, simanzi iliongezeka lakini tukaomba dua na kuondoka,” alisema Halima Yahaya ‘Davina’ aliyekuwa mmoja wa wasanii waliokuwa kwenye msafara huo.

No comments:

Post a Comment