Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, October 20, 2015

Cannavaro: Tulijitakia wenyewe kudroo na Azam

cannavaro-FILEminimizer

Nadir Haroub ‘Cannavarao’.
Sweetbert Lukonge, Dar
TIMU ya Yanga juzi Jumamosi ilipoteza nafasi nyingi za mabao katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, hali hiyo imemsononesha beki na nahodha wa timu hiyo, Nadir Haroub ‘Cannavarao’ ambaye amesema walijitakia wenyewe kudroo na Azam na kila mchezaji anapaswa kulijutia hilo.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Cannavaro alisema katika mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa, Yanga ilipata zaidi ya nafasi nane za kufunga lakini ikatumia moja wakati Azam wao walipata nne na wakutumia moja.

 
“Katika mechi hiyo, tuliwazidi kila kitu Azam na kuna wakati walichanganyikiwa kabisa, lakini tukashindwa kuzitumia vizuri nafasi tulizozipata na kujikuta tukitoka nao sare.
“Kwa hali hiyo hakuna mtu wa kulaumiwa juu ya hili ila ni sisi wenyewe wachezaji na ninaweza kusema tumejitakia wenyewe,” alisema Cannavaro

No comments:

Post a Comment