Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, October 20, 2015

Waangalizi zaidi wa EU wawasili Tanzania

Waangalizi wa uchaguzi

Kikosi hicho ndicho kikubwa zaidi cha waangalizi wa kimataifa Tanzania

Waangalizi wa muda mfupi kutoka Muungano wa Ulaya (EU EOM) wamewasili nchini Tanzania kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Jumapili.
Waangalizi hao 60 waliwasili jijini Dar es Salaam jana na wanatarajiwa kutumwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo kuanzua Jumanne.
Wataungana na waangalizi wa muda mrefu wa muungano huo ambao wamekuwa wakifuatilia maandalizi ya uchaguzi pamoja na kampeni tangu mwisho wa mwezi Septemba.
Waangalizi hao wa muda mfupi wanafikisha 140, jumla ya waangalizi waliotumwa na Muungano wa Ulaya kuangalia uchaguzi huo.

 
"Tutakuwa na waangalizi 140 watakaotembelea vituo vya kupiga kura kwenye maeneo ya mijini na vijijini, kwenye
Mikoa yote, ili kuangalia upigaji na kuhesabiwa kwa kura,” amesema Mwangalizi Mkuu wa EU, Judith Sargentini.
“Waangalizi wetu watafuatilia pia uorodhoshwaji wa matokeo, ambazo ni sehemu muhimu ya tathmini ya jumla ya
EU EOM ya mchakato wa uchaguzi.”
Waangalizi hao wa uchaguzi watakuwa nchini Tanzania hadi Novemba 15 na wanatarajiwa kutoa tathmini ya awali kuhusu uchaguzi huo muda mfupi baada ya kumalizika kwa uchaguzi wenyewe.

No comments:

Post a Comment