Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 22, 2015

Diamond platnumz kutumbuiza kwenye tamasha la BET EXPERIENCE 2015


Lile tamasha kubwa la BET Experience ambalo hufanyika L.A, Marekani wakati wa sherehe za utoaji wa tuzo za BET, linatarajiwa kufanyika Afrika kwa mara ya kwanza mwaka huu na kuitwa BET Experience Africa.
Tofauti na diamond wasanii wengine waliotajwa tayari ni Tamar Braxton, Maxwell, na Flavour na wengine kuendelea kutajwa hivi karibuni
Tamasha la BET Experience Africa ambalo litajumuisha burudani za aina mbalimbali ikiwemo muziki, comedy, mitindo, na mambo mengine mengi limepagwa kufanyika Desemba 12, 2015 jijini Johannesburg, Afrika Kusini.“VIMN Africa and BET are proud to introduce this incredibly successful BET franchise to African audiences for the first time, celebrating so many rich and varied faces of the urban lifestyle experience under one roof.” Alisema makamu wa Rais na mkurugenzi mtendaji wa Viacom International Media Networks ( VIMN) Afrika, Alex Okosi.

Kwa Marekani mwaka huu (2015) tamasha hilo lilifanyika kwa siku 4 kuanzia June 25 hadi siku yenyewe ya tuzo June 28 ikiwa ni mara yake ya 3 kufanyika. BET Experience 2016 ya Marekani imepangwa kufanyika June 23-26, 2016.

No comments:

Post a Comment