Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, October 29, 2015

PICHA:::MSANII LUTENI KARAMA ALIPOFUMANIWA NA MPENZI WAKE

MISS Ruvuma 2006 anayedaiwa kuishi mjini ‘kiujanjaujanja’, Isabellah Mpanda ‘Bella’, juzikati alimfumania Mbongo Fleva, Kalama Bakari ‘Luteni Kalama’ kwa kumkuta live na mchepuko aitwaye Winnie ambaye ni mdogo wa Bella kwa kuchangia mama, Amani lina hatua kwa hatua.
Alipowafumania.
Tukio hilo lilijiri nyumbani kwa Bella, Makumbusho jijini Dar es Salaam baada ya kurejea ghafla kutoka safari ya kimuziki kwenye kampeni za udiwani katika Mikoa ya Iringa na Morogoro.Siku ya tukio, paparazi wetu alikuwa akipita na hamsini zake katika eneo hilo ndipo alipokutana na songombingo hilo ambapo kelele za Bella zilifika nje huku milio ya vyombo kuvunjwa ikitawala.Paparazi wetu alitia nanga kwenye nyumba hiyo ambapo majirani nao walianza kufika na kumkuta Bella akimshushia kipondo mdogo wake huyo huku akianika uhusiano wao.
...Akivua pete ya uchumba aliyovishwa.
“Huyu ni mdogo wangu kabisa. Tunachangia mama. Nilimleta hapa kwa ajili ya muziki. Sasa mimi nikiwa safarini, kuna mtu alinipigia simu na kuniambia Winnie anaingia na kulala na Kalama chumbani kwangu.
“Sikutaka kumwambia Kalama kuhusu nilichoambiwa, nikaamua kuja ghafla ili nithibitishe. Kumbe kweli. Yaani mdogo wangu kabisa ananifanyia hivi jamani?” alihoji Bella huku akivua pete ya uchumba aliyovalishwa na Kalama na kumtupia.

Mazingira ya eneo la tukio, sakafuni kulikuwa na vipande vya chupa ambavyo vilitokana na Bella kuvunja glasi kwa lengo la kutaka kumpasua kichwani mdogo wake.
Juzi, paparazi wetu alifika tena nyumbani hapo na kuambiwa na msichana mmoja kwamba, Kalama aliondoka baada ya tukio huku Winnie akipokea msamaha wa ‘damu nzito kuliko maji’.Bella alipopigiwa simu na kuulizwa hatima yake na Kalama, alisema: “Mimi na Kalama basi japo ananipigiapigia simu kuniomba msamaha.”
Kalama hakupatikana kuzungumzia hilo.No comments:

Post a Comment