Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 18, 2015

MAPIGANO MAKALI YAZUKA TENA PARIS UFARANSA

Askari Polisi wakijiandaa kufanya doria katika Kitongoji cha Saint-Denis
Wakiingia kwa pamoja.Mapigano yakiendelea.Wanajeshi nao wakiiarisha ulinziPolisi katika doria

 
Mashambulizi.Wakiingiaharakati zikiendelea.
Wakiwatoa wakazi wa eneo hilo.Polisi wakipanga.Mapigano.
Mtuhumiwa Salah Abdeslam.
Mtuhumiwa Abdelhamid Abaaoud.
Paris, UfaransaHALI si shwali! Gaidi mwanamke aliyevalia mabomu akitaka kujilipua ili awauwe askari, amejipiga risasi mwenyewe huku gaidi mwingine akiuawa wakati wa makabiliano na Polisi na Wanajeshi zaidi ya 100 katika Kitongoji cha Saint-Denis kaskazini mwa Mji wa Paris nchini Ufaransa leo asubuhi. 

Mwanamke huyo alianza kwa kuwashambulia kwa risasi askari hao waliokuwa wamezingira nyumba ya wageni huko Saint-Denis anamosadikiwa kujificha Salah Abdeslam (26), mtuhumiwa mmoja kati ya tisa waliohusika kwenye shambulio la Paris, Ijumaa iliyopita na kuuwa watu 129. 

Wakati wa majibizano ya risasi na askari, mwanamke huyo akiwa na bunduki aina ya AK-47alimpiga mtuhumiwa mwingine wa ugaidi aliyekuwa dirishani na kumuua huku akimjeruhi askari mmoja na kuuwa mbwa mmoja wa polisi kabla ya kujipiga risasi mwenyewe. 

Mashuhuda wa tukio la Ijumaa wanasema, aliyetekeleza shambulio katika Ukumbi wa Bataclan alionekama kuwa ni mwanamke. 
Polisi wamekamata watu watano kwenye tukio hilo na kuwaweka chini ya ulinzi ili kuwahoji Zaidi.

No comments:

Post a Comment