Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 12, 2015

Onyesho la Coke Studio lazidi kupaisha mafanikio yangu-Ali Kiba

 Mwanamuziki Ali Kiba akionyesha machachari yake katika onyesho la Coke studio akiwa na mwanamuziki wa Kenya Victoria Kimani
Mwanamuziki wa Tanzania Ali Kiba akiwasha moto katika onyesho la Coke studio
Awataka wasanii wachanga kujituma ili waweze kushiriki kwenye onyesho kama hili


Mwanamuziki nguli wa miondoko ya Bongo Fleva nchini Ali Kiba amesema moja ya mafanikio anayojivunia nayo katika kazi ya muziki kwa mwaka huu ni ushiriki wake katika onyesho la Coke Studio msimu wa tatu.

Ali Kiba ambaye amefanya kolabo kwa kushirikiana na mwanamuziki wa kike anayetamba katika anga ya muziki wa Bongo Fleva nchini Kenya Victoria Kimani amesema katika mahojiano hivi karibuni kuwa anajivunia kuwa miongoni mwa wanamuziki wanaoshiriki kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio unaoendela ambapo kwa hapa nchini onyesho hilo linarushwa na luninga ya Clouds kila Jumamosi saa 12 jioni na kurudiwa saa tatu usiku.

Anasema ushiriki wake kwenye ni bonge la mafanikio
kwani rekodi yake imezidi kuongezeka katika anga la kimataifa na ameweza kujiongezea washabiki ambao wafuatilia onyesho hili kupitia luninga,vyombo vya habari na mitandao ya kijamii.

Mbali na kuongelea mafanikio ya kupata washabiki amesema kuwa amefurahi kufanya kolabo (mash-up) na msanii wa nje ya nchi kwa kuwa ameweza kujifunza mengi kupitia ushiriki wake kwenye Coke Studio.
Alisema onyesho la Coke Studio linadhihirisha kuwa muziki wa Bongo Fleva unazidi kukua na kuwa maarufu sehemu mbalimbali barani Afrika kutokana na jinsi linavyofuatiliwa na idadi kubwa ya watu hususani vijana.

Aliwataka wanamuziki wachanga wanaochipukia kufanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha wanapata mafanikio.

“Fani ya muziki inazidi kukua kiasi kwamba wakati wa kufanya muziki wa ndani tu imekwisha na inabidi kuvuka mipaka na kufanya kolabo(mash-up) kama hizi za Coke Studio zinasaidia kupata uzoefu na kufungua milango ya mafanikio”.Alisema.

Alimalizia kwa kuwapongeza wanamuziki wenzake kutoka Tanzania ambao wako nao katika msimu wa Coke Studio mwaka huu. Wanamuziki hao ni Ben Pol ambaye amefanya kolabo (mash-up) na Wangechi kutoka Kenya, Fid Q ambaye amefanya kolabo (mash-up)Maurice Kirya na Vanessa Mdee ambaye amefanya kolabo (mash-up) na mwanamuziki 2face kutoka Nigeria.


Onyesho la Coke Studio linarushwa na luninga ya Clouds kila Jumamosi saa 12 jioni na kurudiwa saa 3 usiku. Pia unaweza sikiliza show kwenye redio ya Clouds FM kila jumamosi saa 4 asubuhi. 

No comments:

Post a Comment