Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, November 12, 2015

RAY C ATOA KAULI BAADA YA PICHA ZAKE KUSAMBAA MITANDAONI

Kumeenea picha mbaya na stori kuhusu Ray C na kilichotokea jana kwenye account yake ya Instagram, leo Soudy Brown kampata na kajibu yote ilivyokuwa.

Ray C amesema zile picha ni zake private ambazo alizihifadhi kwenye simu yake, lakini kwa bahati mbaya simu yake imepotea na aliyeiba simu ndio aliamua kuanza kupost picha alizokuta kwenye simu ya Ray C.

Ray C amesema alituma email kwa wamiliki wa Instagram ili waifungie account hiyo, lakini anaomba radhi kwa kilichotokea kwa sababu sio yeye aliyepost picha hizo.Niombe tu msamaha maana sijui hata naanzaje kuelezea… naomba tu waelewe kwamba simu nimeibiwa na mtu ambaye amefanya hivyo namjua na nimeripoti Polisi.. naomba tu msamaha“- hii ni sehemu ya maneno ya Ray C alipokuwa kwenye U Heard na Soudy Brown .

No comments:

Post a Comment