Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 18, 2015

SAKATA LA MKUU WA MAJESHI MH DAVIS MWAMUNYANGE SERIKALI YAKATA RUFAA KUPINGA MAAMUZI


Upande wa Jamhuri katika kesi inayomkabili mwanafunzi wa Taasisi ya Teknolojia Tanzania (DIT), Benedict Ngonyani, anayetuhumiwa kusambaza taarifa katika mtandao wa kijamii wa Facebook kuwa Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Jenerali, Davis Mwamunyange, amelishwa sumu, umewasilisha mahakamani kusudio la kukata rufaa kupinga mshtakiwa huyo kupewa dhamana.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, iliyoketi chini ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage, ilitengua hati ya kuzuia dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo iliyowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP). 



Kabla ya uamuzi huo, hakimu alisikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili na alikubaliana na maombi ya utetezi ya 

kumpa dhamana kwa kuwa sababu za DPP kuzuia dhamana hiyo hazikuwa na msingi wa kisheria.
Wakili wa Serikali Mkuu, Theophil Mutakyawa aliwasilisha kusudio hilo jana saa 7:00 mchana, kwamba upande wa Jamhuri haujaridhika na uamuzi wa mahakama kutengua hati ya DPP.
Pia, kupitia kusudio hilo, upande wa Jamhuri unapinga Mahakama ya Kisutu kutengua hati hiyo na kwamba haina mamlaka ya kuoindoa kwa kuwa huondolewa na DPP ama kesi inapomalizika na kutolewa hukumu.
Awali hakimu alisema mshtakiwa ni mwanafunzi na shtaka analoshtakiwa nalo linadhaminika kwa hiyo haoni haja ya kukosa masomo yake ya darasani
Katika kesi hiyo, inadaiwa Septemba 25, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alisambaza taarifa za uongo kinyume cha Sheria ya Makosa ya Mtandao kifungu cha 16 ya mwaka 2015 kuwa Jenerali Mwamunyange amenyweshwa sumu.

No comments:

Post a Comment