Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, November 18, 2015

WALIOJENGA BILA KUFUATA TARATIBU ZA UJENZI NYUMBA ZAO KUBOMOLEWA KATIKA MANISPAA YA KINONDONI

 Mkutano wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Waandishi wa Habari kuhusu zoezi la ubomoaji wa nyumba Manispaa ya Kinondoni (kuanzia kushoto) Mhandisi wa Manispaa ya Kinondoni, Bw. Baraka Mkuya, Kamishna wa Ardhi Tanzania Dkt. Moses Kusiluka na Kamishna wa Ardhi Msaidizi kanda ya Dar es salaam Bw. Methew Nhonge.



Manispaa ya Kinondoni kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , kama msimamizi na mtekelezaji wa sera ya Taifa ya Ardhi, inakusudia kuendesha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa bila kufuata taratibu za ujenzi.  
Maeneo yaliyotengwa mijini kwa matumizi ya umma ikiwa ni pamoja na maeneo ya wazi, njia za miundombinu na huduma nyinginezo za umma, mara kwa mara hutumiwa vibaya au kuvamiwa na waendelezaji binafsi hivyo kuukosesha umma manufaa yaliyokusudiwa.

Tamko Na. 6.6.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:  
i. Serikali itahakikisha kwamba maeneo yote mijini yaliyotengwa kwa shughuli za umma yanatumika kwa shughuli zilizokusudiwa na yanalindwa ili yasivamiwe.

Tamko Na. 8.2.1 la Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995:  
ii. Serikali za mitaa zitawajibika kushirikiana na Wizara ya Ardhi kuhakikisha usimamizi mzuri wa ardhi katika maeneo yao.


Sera ya Taifa ya Ardhi imebainisha sababu inayopelekea Wizara kushirikiana na Manispaa ya Kinondoni kuendesha zoezi hili la ubomoaji. Ubomoaji huu utahusisha nyumba zote zilizojengwa  
a) Bila kibali cha ujenzi  
b) Bila kufuata michoro ya mipango miji  
c) Bila kufuata matumizi ya ardhi (maeneo ya wazi)

Zoezi hili la ubomoaji litaendeshwa na Manispaa ya kinondoni na Wizara ya Ardhi itasimamia sera za ardhi na taratibu za uendelezaji kuhakikisha zinafuatwa na kila mmiliki wa ardhi.  
Maeneo ambayo ujenzi wake umekiuka matumizi kusudiwa na yatahusika na ubomoaji huu ni Mbezi, Tegeta, Bunju, Mwenge na Kinondoni – Biafra. Kazi hii inatarajiwa kufanyika kwa siku tatu kuanzia jumatano tarehe 18/11/2015 hadi ijumaa tarehe 20/11/2015.

No comments:

Post a Comment