Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, November 23, 2015

WATU 16 WAJERUHIWA KWA RISASI MAREKANI

Marekani (7)Majeruhi wakikimbizwa hospitali.Marekani (6)Polisi wakiwasaidia waathirika wa tukio hilo.
Marekani (5)Umati wa watu kabla ya tukio hilo.Marekani (4)Hali ilivyokuwa eneo la tukio.


 
Marekani (3)Polisi wakiimarisha ulinzi.Marekani (2)Marekani (1)…Pakiwa pamepooza.
New Orleans, Marekani
WATU wapatao 16 wakiwa kwenye mkusanyiko wamejeruhiwa baada ya kufyatuliwa risasi na watu wasiojulikana mjini New Orleans nchini Marekani.
Tukio hilo limetokea jana jioni amapo watu wapatao 500 walikuwa wamekusanyika kwenye makundi mawili katika bustani ya Bunny Friend Park mjini New Orleans. Kundi la kwanza walikwenda kutazama video iliyokuwa ikiandaliwa bustanini hapo, na kundi la pili wakienda kwenye gwaride la wakazi wa mtaa huo ndipo kikundi kingine cha watu watano wasiofahamika wenye silaha akiwemo mwanamke mmoja walizuka na kuanza kuwashambulia umati huo kwa kuwarushia risasi  kisha kujeruhi 16.
Baada ya taharuki hiyo polisi wa eneo hilo walifika na kuanza kujibizana nao risasi ndipo wakaamua kukimbia, polisi waliwachukua majeruhi hao na kuwapeleka hospitali.
Shuhuda mmoja wa tukio hilo amekaririwa akisema kuwa, mmoja kati ya wavamizi hao alijipenyeza katikati ya umati huo na kufyatua risasi mara 10, baadaye waliingia watu wanne wakiwa na silaha pia, nao wakaanza kushambulia umati huo.

No comments:

Post a Comment