Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, January 27, 2016

ASKARI POLISI WOTE MAKAMBINI WANALIPIWA UMEME NA SERIKALI - JESHI LA POLISI


 Katika gazeti la Tanzania Daima ukurasa wa 5, toleo namba 4070 la tarehe 25 Januari, 2016, lilichapisha habari yenye kichwa cha habari Polisi “waisoma” namba. Sehemu ya taarifa hiyo inaeleza kuwa askari Polisi hivi sasa wanatakiwa kujilipia gharama za umeme. 

Jeshi la Polisi nchini, linakanusha vikali taarifa hiyo kwamba siyo sahihi. Ukweli ni kwamba askari polisi wote makambini wanalipiwa umeme na serikali,  ikiwemo wale ambao nyumba zao zimefungiwa luku kama njia ya kuboresha huduma na matumizi sahihi ya umeme. Baada ya askari kununua umeme hutakiwa kuwasilisha stakabadhi ya malipo ya umeme kwa ajili ya kurudishiwa kiasi cha fedha walichonunulia umeme kila mwisho wa mwezi. 
Aidha, habari iliyochapishwa na Tanzania Daima ililenga kupotosha umma na mwandishi wa habari hiyo hakutafuta ufafanuzi kutoka kwenye mamlaka husika. 

 
Kufuatia hali hiyo, Jeshi la Polisi nchini, linamtaka mhariri wa gazeti la Tanzania Daima na waandishi wake wa habari kuwa makini na habari wanazoziandika hasusani taarifa zinazohusu vyombo vya ulinzi na usalama ili kuepuka madhara ya kiusalama yanayoweza kutokea kutokana na habari wanazozitoa zisizo na usahihi.

Imetolewa na:-
Advera Bulimba -SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi,
Makao Makuu.

No comments:

Post a Comment