Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 26, 2016

NINI MAANA YA TEZI DUME NA CHANZO CHAKE


MAKALA YA TEZI DUME

(Kutoka kwa Dr. Mackfallen Giliard)

Kwa kawaida mwanaume ana matezi mawili yanayohusiana na uzazi. Tezi la kwanza linaitwa cowper's gland

Kazi ya hili tezi ni kutoa majimaji ya kuondoa acid iliyoachwa kwenye njia ya mkojo na mkojo. Kwa wanaume wanajua hivi ni vile vimajimaji vinavyoaanza kabla ya kuja mzigo wenyewe

Hii inatokana na ukweli kuwa mbegu za kiume zinaishi kwenye mazingira ya Alkali. Tezi la pili ni Prostate.Kama linavyoonekana hapo kwenye picha hapo juu hili tezi lipo kwenye shingo ya njia ya mkojo. Kwa hiyo basi tezi hili likileta mishkeli tu kidogo linaziba njia ya mkojo na mtu kushidwa kukojoa. Kazi ya hili tezi ni kutoa majimaji kwa kikwetu tunaita Shahawa. Huu ute mzito una kazi kuu mbili. Kazi ya kwanza ni 

kuwezesha mbegu ziweze kuogeleaaa na kubembeaa na kazi ya pili ni kuondoa hali ya acidi kwenye uke na kuweka hali ya Alkali (hii ndio maana tukaita chumvini shauri ya acid) kwani mbegu zinaweza kuishi kwenye acid.

Kwa kawaida tezi dume linatakiwa kuwa na urefu wa centimetres 2.5 ukilipima kwa kupitia njia ya Haja kubwa Kwa kitaalamu per rectal examination. Na vile vile linatakiwa liwe laini na lililo free bila kujishikia sehemu yeyote. Kwa minajiri hiyo basi njia Rahisi na inayotumika kwenye nchi maskini ni hiyo ya kufanya PR. Kidole ingawaje kulingana ma technologia ya kisasa kuna njia zingine zitatumika I kiwepo urinoscope ambayo kifaa chenye kamera kinaingizwa kwenye njia ya mkojo kwenda kuangalia hilo tezi dume.Kwenye kisababishi cha kwanza ni umri cha pili bado kuna mkanganyiko kutoka kwa wataalamu wengine wanasema ukifanya sana ngono celi za hili tezi zinakuwa kwa vile linakuwa na kazi kubwa sana kwenye kuzalisha Shahawa kwa hiyo linaongezeka. Wengine wanasema ukifanya sana unapunguza manii. Ingawaje hata usipofanya huwa wanaume wengi wanapata njozi pevu na kushusha mzigo

Sasa basi kwa Tanzania kwa sasa ni kama kuna kampeni ya kupima tezi dume na kama nilivyoeleza hapo juu njia rahisi na ya gharama nafuu ni hiyo ya PR kidole ndio maana tunaambiwa wanaume tusiogope kidole.Tezi dume likikua kuzidi ukubwa wake unaotakiwa linaziba njia ya kutolea mkojo kwani lipo kwenye shingo ya njia ya mkojo. Mkojo ni sumu kali sana mwilini. Kwanza kibofu kikikijaa mkojo kinauma sana maumivu makali sana. Na mkojo ukiendelea kubakii mwilini utarudi kwenye figo them mwilini na kumsababishia mtu sumu kali uraemia.

No comments:

Post a Comment