Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, January 31, 2016

TAZAMA PICHA YA MANOWARI KUBWA YA JESHI LA MAREKANI

Jambo moja ambalo watanzania na watu wengi duniani hawafahamu ni uwezo wa jeshi la anga wa Marekani. Ingawa Siri kamili ya uwezo wa jeshi hilo wanayo wenyewe lakini kwa taarifa ambazo nimezipata kwa msaada wa mitandao mbali mbali ya internet nguvu za jeshi la marekani zinatisha.
====Taarifa zinaonyesha kuwa jeshi la anga la Marekani linamiliki ndege zisizopungua 14,500 zinazofanya kazi. Idadi hii ya ndege ni kubwa na huenda hakuna nchi duniani 

 
ambayo inaweza kufikia idadi za ndege za jeshi hilo. Aidha wakati urusi ikitajwa kumiliki silaha nyingi sana za kivita lakini Marekani ndo yenye silaha kali na nyingi zaidi
===Katika ndege hizo, Marekani inamiliki ndege 74 aina ya B52 ndege zenye enjini nane, ni ndege ambazo ndizo ndege kubwa zaidi duniani katika historia ya ndege za kivita. Ndege hizo ambazo kubwa kuliko ndege zote za kivita duniani ambazo pia ni muundo ambao haziwezi kudondoshwa kirahisi ni maalumu kwa mashambulizi mazito yakiwemo mashambulizi ya mabomu na rocket
Aidha katika idadi hiyo ya ndege inazomilikiwa ndege 174 zimetengenezwa kuwa ushirkiano wa Marekani na kanada, 118 Uingereza na Marekani, 13 Marekani na Italia. Ndege 20 ni za kirusi, Ndege 142 ni za Kifaransa, ndege 43 ni za kiingereza, 23 za kikanada, 4 za Poland, 2 za Kiholanzi, 13 za kihispania, 2 za kiswitzerland. Ndege nyingine zimetengenezwa na marekani wenyewe
=== ndege hatari zaidi ambazo idadi yake haijafahamika zimetengenezwa Israel na hizo hazijawahi kutumika Zipo zinasubiri kiwake...

No comments:

Post a Comment