Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 26, 2016

VIFUNGU vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 vyapingwa mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

 Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi akizungumza jambo na Wakili wakujitegemea, Jebra Kambole baada ya kutoka Mahakama Kuu ambako wamefungua hauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa.
 Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi akizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutoka Mahakamani hapo ambapo wamefungua shauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa, ambapo wameona hiyo ni kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi katika jamii. 

 
Wakili wakujitegemea, Jebra Kambole kizungumza na Waandishi wa Habari nje ya Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kutoka Mahakamani hapo ambapo wamefungua shauri la Kikatiba la kupinga sheria ya ndoa kifungu cha 13 na 17 vinavyoruhusu mtoto wa kike chini ya miaka 18 kufunga ndoa, ambapo wameona hiyo ni kumnyima mtoto wa kike haki yake ya msingi katika jamii.


Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
VIFUNGU vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18 vyapingwa mahakama kuu leo jijini Dar es Salaam.

Vipengele vinavyopingwa ni kifungu cha sheria cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa (CAP 29 R.E 2002), sheria inayotoa mwanya kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakana na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi ambayo ni kinyume na ibara ya 13, 12 na 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 19977 zinazotoa haki ya usawa mbele ya sheria kutokubaguliwa, kuheshimu utu wa mtu na uhuru wa kujieleza.

Kesi ya kupinga vifungu  vya sheria ya ndoa vinavyoruhusu mtoto wa kike kuolewa chini ya miaka 18  ni keshi ya kikatiba yenye namba tano ya mwaka 2016 iliyofunguliwa na Mwanaharakati wa haki za binadamu, Rebeca Gyumi na kusimamiwa na wakili Jebra Kambole wa Law Guards Advocate.

Akizungumza na waandishi wa jijini Dar es Salaam leo Mwanaharakati wa Haki za Binadamu, Rebeca Gyumi  ameomba mahakama kuu kufutia mbali vifungu vya sheria hivyo na kupandisha umri wa chini wa kuoa  kwa wanaume na kuolewa kwa wanawake kuwa ni miaka 18.

Aidha Rebeca amesema kuwa  ndoa za utotoni kwa wasichana ni ukiukwaji wa haki za binadamu pia kuzaa kwa msichana akiwa na umri mdogo ni chanzo kikubwa cha matatizo ya Fistula na vifo vingi vya wajawazito.Chanzo Mtaa Kwa Mtaa Blog

No comments:

Post a Comment