Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, January 26, 2016

WAZAZI MKOANI MWANZA WASIKITIKA ELIMU BURE KUWABAGUA WANAFUNZI WA ELIMU YA WATU WAZIMA.

Wazazi na Walezi wa Wanafunzi wanaosoma kitengo cha elimu ya Watu Wazima katika Shule ya Sekondari Pasiansi iliyopo Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, wameiomba Serikali kuondoa ada kwa wanafunzi hao ili nao waweze kunufaika na mpango wa elimu bure nchini.

Wazazi hao wametoa ombi hilo hii leo baada ya kumalizika kwa kikao baina yao na uongozi wa Shule hiyo pamoja na Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza, sanjari na viongozi wengine akiwemo diwani wa Kata ya Pasiansi pamoja na Afisa elimu Sekondani katika Manispaa ya Ilemela.


Malalamiko yao yanafafanua kwamba, hawakuambiwa tangu awali kuwa watoto wao wanasoma elimu ya Watu Wazima, malalamiko ambayo hata hiyo yamekanushwa na Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Joseph Bangirana.

Awali wazazi hao walisema kuwa hawako tayari kulipa ada kwa ajili ya watoto wao wanaosoma katika shule hiyo, jambo lililomlazimu Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza kueleza bayana kwamba, wanafunzi wa Elimu ya Watu Wazima hawanufaiki na mpango wa elimu bure nchini kwa kuwa Serikali haitoi ruzuku kwa ajili yao.

Ufafanuzi huo ukaungwa mkono na Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela.

Wakati ufafanuzi huo ukitolewa, mmoja wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo ya Pasiansi akasisitiza suala la wao kuondolewa ada ili nao wanufaike na mpango wa elimu bure.

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima katika shule ya Sekondari Pasiansi, kilianzishwa Mwaka 2014 na kuanza kupokea wanafunzi waliomaliza darasa la Saba waliokuwa na ufaulu wa chini ya Wastani wa pinti 100 kwa lengo la kuwapa fursa ya kupata elimu ya Sekondari ambapo mbali na michango mingine, wanafunzi hao wanalipa ada ya Shilingi Laki Moja na Elimu Hamsini kwa mwaka.
Kikao Kikiendelea
Mwalimu Juma Kasandiko ambae ni Afisa Elimu Sekondari katika Manispaa ya Ilemela akitoa ufafanuzi kwa Wazazi juu ya suala la Elimu Bure nchini.
Malimi Joram ambae ni Mkufunzi Msaidizi kutoka Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza
Andrea Swai kutoka Elimu ya Watu Wazima Mkoani Mwanza akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Mwalimu Joseph Bangirana ambae ni Mkuu wa Shule Pasiansi Sekondari akitoa ufafanuzi katika kikao hicho
Diwani wa Kata ya Pasiansi Mhe.Japhesi Joel Rwehumbiza akitoa ufafanuzi wake. Amewapongeza wazazi kwa kufuatilia masuala ya elimu yanayowahusu
Mdau wa Elimu Mkoani Mwanza, Peter Matonyi akitoa mchango wake juu ya suala la elimu bure kwa wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pasiansi Mkoani Mwanza, Emmanuel Masuka akifafanua jambo
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Mmoja wa Wazazi akiwasilisha malalamiko yake juu ya suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Wanalalamikia suala la elimu bure kuwabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima
Elimu bure inawabagua wanafunzi wa elimu ya watu wazima

No comments:

Post a Comment