Ajali mbaya ya barabarani imetokea mkoani Tanga asubuhi Ya Leo wakati Basi la Kampuni ya Simba Mtoto ya Tanga lilipogongana na Lori uso kwa uso katika eneo la Pangamlima Wilayani Korogwe mkoani humo,taarifa za awali kutoka eneo la tukieo zinaeleza kuwa watu 10 wanahofiwa kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya atika ajali hiyo.
Globu ya Jamii bado inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu ili kupata idadi kamili ya waliopoteza maisha.Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi-AMIN
No comments:
Post a Comment