Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, February 8, 2016

DR CONGO WATWAA UBINGWA WA KOMBE LA CHANTimu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametwaa ubingwa wa kombe la Chan baada ya kuichapa Mali kwa mabao 3-0.
Mabao ya washindi ya Congo yalifungwa na Meshak Elia aliyefunga bao mbili wakati Jonathan Bolingi alifunga goli jingine kukamilisha ushindi wa DR Congo.
Mwaka 2009 DR Congo ilichukua kombe hilo kwa mara ya kwanza kwa kuifunga Ghana kwa magoli 2-0 kwenye mchezo wa fainali.


Kwenye mashindano ya mwaka huo Tanzania pia ilishiriki michuano hiyo lakini ilitolewa kwenye hatua ya makundi.

DR Congo imechukua kitita cha dola za Marekani 750,000 wakati mshindi wa pili ambayo ni timu ya Mali yenyewe ikiondoka na dola za Marekani 400, 000 huku mshindi wa tatu timu ya taifa ya Ivory Coast ikijishindia dola 250,000

No comments:

Post a Comment