Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, March 8, 2016

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AKUTANA NA WAWEKEZAJI KUTOKA KOREA NA INDIA LEO


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Profesa Choi Oe Chool Rais wa GLOBAL SAEMAUL DEVOLOPMENT NETWORK ya Jamhuri ya Korea, Wakati Rais huyo na Ujumbe wake alipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March 08,2016, kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia juu ya kukuza na kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Uchumi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea ratiba ya mpango wa maendeleo wa Jumuiya ya GLOBAL SAEMAUL UNDONG kutoka kwa Profesa Choi Oe Chool Rais wa GLOBAL SAEMAUL DEVOLOPMENT NETWORK ya Jamhuri ya 

 
Korea, Wakati Rais huyo na Ujumbe wake walipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March 08,2016, kwenye mazungumzo yao Viongozi hao wamezungumzia juu ya kukuza na kuendeleza ushirikiano wa kimaendeleo katika Nyanja mbalimbali ikiwemo Uchumi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya GLOBAL SAEMAUL DEVOLOPMENT NETWORK ya Jamhuri ya Korea, Wakati Ujumbe huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March 08,2016.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Ujumbe wa Uwekezaji katika Nyanja wa Viwanda vya Sukari kutoka Kampuni ya RAK INTERNATIONAL LTD ya India, Wakati Ujumbe huo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March 08,2016, kwa lengo la kutaka kuwekeza Viwanda vya Sukari hapa Nchini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia mpango wa maendeleo wa Viwanda ulioandaliwa na Kampuni ya RAK INTERNATIONAL LTD ya India, Wakati Ujumbe wa Kampuni hiyo ulipofika Ofisini kwa Makamu wa Rais Ikulu Dar es Salaam Leo March 08,2016, kwa lengo la kutaka kuwekeza Viwanda vya Sukari hapa Nchini. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya RAK INTERNATIONAL LTD Bw. Sundeep Patil. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment