![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhmmWxh7wXVbDphklPofexVyWHGI2K1BhfVEJkckrDBIzdGT78_AhQXChbY5b1Be4On6cCs47qUTYTmE6G1G1rzPDYllY_s3SaXBb8iehkgDFBIu25o_pUwPcm1oEm4A4GBMmgxdOwsQw0/s640/Charles+Boniface+Mkwasa.jpg)
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premieum Lager, Charles Boniface Mkwasa
leo ametangza kikosi cha wachezaji 25 kwa ajili ya mchezo wa kuwania kufuzu kwa
fainali za Mataifa Afrika (AFCON) dhidi ya Chad, Machi 23, 2016 mjini Djamena.
Akiongea na waandishi wa habari wakati akitangaza kikosi
hicho, Mkwasa amewaomba wachezaji aliowaita katika kikosi hicho, kujiweka fit
katika mazoezi wanayoyafanya katika vilabu vyao, kwani hakutakua na muda wa
kufanya mazoezi kwa ajili ya mchezo huo wa ugenini.
“Ligi Kuu ya Vodacom, michuano ya CAF (CL, CC) inachezwa
wikiendi ya tarehe 18-20 Machi, hivyo wachezaji wote watakua na majukumu katiak
timu zao, muda wa kufanya mazoezi kwa pamoja kwa ajili ya mchezo huo
hautakuwepo, ndio maana nasisitiza wachezaji niliowachagua wahakikishe
wanajilinda wenyewe kwa kuwa fit wanapokuja kwenye safari ya mchezo huo wa
machi 23, 2016” alisema Mkwasa
Wachezaji walioitwa Taifa Stars ni magolikipa Aishi Manula
(Azam FC), Ally Mustapha (Young Africans) na Shaban Kado (Mwadui FC), walinzi
ni Juma Abdul, Haji Mwinyi, Kelvin Yondani (Young Africans), Shomari Kapombe,
Erasto Nyoni, David Mwantika (Azam FC) na Mohamed Hussein (Simba SC).
Viungo Himdi Mao (Azam FC), Ismail Juma (JKU), Jonas Mkude,
Said Ndemla, Mwinyi Kazimoto (Simba SC), Mohamed Ibrahim, Shiza Kichuya (Mtibwa
Sugar), Farid Mussa (Azam FC), Deus Kaseke (Young Africans).
Washambuliaji ni Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk), Thomas
Ulimwengu (TP Mazembe), John Bocco (Azam FC), Elias Maguri (Stand United),
Jeremia Mgunda (Tanzania Prisons) na Ibrahim Hajibu (Simba SC).
No comments:
Post a Comment