skip to main |
skip to sidebar
HALI YA MTOTO CESILIA NI MBAYA ARUDI BILA KUFANYIWA OPERESHENI.
Hapa
Mtotokama anavyoonekana katika picha hii
Mtoto Cecilia alitangazwa hivi karibuni na Vituo mbali mbali vya habari
akiomba msaada wa kusaidiwa pesa za matibabu ambazo zingeweza
kumwezesha kufanyiwa operesheni ya moyo ambao umempelekea mpaka Tumbo
lake kuvimba kama unavyoliona.
Taarifa za Cecilia ziliweza kutolewa na Miss Tanzania wa mwaka 2006 Bi
.Hoyce Temu pale alipoamua kujitokeza na kumtangaza Cecilia akiomba
msaada huo. Wasamaria wema walijitokeza na kumsaidia Cecilia mpaka
akaweza kwenda India kwa matibabu, cha kusikitisha sana ni kwamba
matibabu yake kwa njia ya operesheni yameshindikana kutokana na moyo
wake kwa upande mmoja kuathirika na sumu ambayo madaktari wa India
wamesema inasababishwa na Sumu ambayo ipo kwenye Mihogo, sumu hiyo
huwaathiri sana watoto wenye umri kama wake.
Kwa hiyo imekuwa ni vigumu kumfanyia operesheni hiyo, wakashauri atumie
dawa tu ili kuweza kuitoa sumu hiyo, Mtoto Cecilia mpaka sasa hali yake
sio nzuri anawaomba watanzania mumuombee ili aweze kupona na aweze
kutimiza azma yake ya kuwa Mwalimu. Watanzania tunashauriwa tukiona
hali ambayo ni tofauti kwa watoto wetu tuwawaishe Hospitali mapemakwa
uchunguzi tunaweza tukawahepusha na hali kama hii aliyofikia Cecilia.
No comments:
Post a Comment