JESHI la polisi mkoani
Iringa
limemkamata mwanahabari Jerry Mulo(pichani) kwa tuhuma za kudaiwa
kutaka kuwapiga picha askari wa kikosi cha usalama barabarani eneo la
ukaguzi wa magari (check point) Igumbilo Manispaa ya Iringa.
Kaim
kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Donald Mashambara alimeuthibitishia
mtandao huu juu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo na kuwa hadi majira
ya saa 10 za jioni ya leo alikuwa bado akihojiwa na polisi toka majira
ya saa 5 asubuhi alipokamatwa .
Mashabara alisema kuwa sababu ya
mwanahabari huyo kukamatwa ilitokana na hatua yake ya kudaiwa kuwapiga
picha askari wa usalama barabarani wakati wakiwa kazini.
Alisema kuwa Mulo alikamatwa majira ya saa 5 .30 asubuhi leo wakati akiwa safarini kutoka jijini
Dar es Salaam kwenda mkoani
Mbeya.
Kaimu kamanda huyo alisema kuwa Mulo ambaye alikuwa akisafiri na
basi la Sumry baada ya kufika katika eneo
hilo
la Igumbilo akiwa na wenzake wawili alishuka kwa madai kuwa basi hilo
lilikuwa limejaza abiria na yeye kuamua kurudi hadi kituo cha ukaguzi
cha Igumbilo na kuanza kupiga picha askari polisi kwa kutumia simu yake
yenye kamera.
"kutokana na hatua ya mwanahabari huyo kupiga
picha askari ndipo walipoamua kumkamata na kumfikisha kituo cha polisi
kwa mahojiano zaidi ili kujua sababu ya kuwapiga picha askari"
Alisema
Mashambala kuwa baada ya mahojiano na upekuzi uliofanywa na polisi
katika kamera ya mwanahabari huyo walibaini kuwa hakukuwa na picha
yoyote ambayo ilikuwa imepigwa na hivyo kulazimika kumwachia huru.
No comments:
Post a Comment