BARAZA la wazee la klabu ya Yanga limesikitishwa na kauli za kejeli na zenye kuwadhalilisha alizozitoa mwenyekiti wa klabu hiyo Lloyd Nchunga juzi, hivyo kuanzia sasa wamemwachia aendelee na timu hiyo.
Hatua
hiyo inafuatia Nchunga kudai kuwa wazee hao walikurupuka na hawezi
kukabidhi kwa wahuni, pia sehemu ambapo hana uhakika na usalama, huku
akihofu timu hiyo kuhudumiwa na wauza dawa za kulevya.
Wakizungumza na mamapipiro blog leo
asubuhi wazee hao wakiongozwa na katibu wao Ibrahim Akilimali walisema
kwamba hawakukupupuka kutangaza kuichukua timu bali walikubaliana na
Nchunga, lakini wanashangaa baadaye kuwageuka.
“Hatukukurupuka
kuongea vile, ilikuwa ni ridhaa ya Nchunga, tulikuwa sahihi kutokana na
mapenzi yetu na timu, pamoja na kuwa uongozi ndio una haki
tuliikubaliana kuichukua timu kwa lengo la kuhakikisha inaifunga Simba,
tunafanya usajili wa uhakika na kurejesha nidhamu,”alisema.
“Ni
ajabu kwa Nchunga kututamkia sisi wauza unga, inamaana mama Fatma
Karume, Francis Kifukwe, Seif Ahmed, Abdallah Binkleb na Yusuf Manji ni
wauza unga?
...hivi
Nchunga anajua umuhimu wa hawa watu ndani ya Yanga,tena kwa mshangao
mkubwa amediriki hata kutuma watu wamzuie kuingia klabuni mzee Kitundu (Jabir)ambaye alishiriki kuijenga klabu,”alisema Mzee Akilimali.
Naye
mjumbe wa baraza hilo, Yussuf Mzimba pamoja kusikitishwa na kauli za
Nchunga, alisema Yanga ina wenyewe na kwamba ukifuga kuku wengi lazima
utapata aliye kisirani ambao wanajifanya wanajua kumbe si lolote.
“Tunataka
serikali iangali watu kama hawa, Nchunga hawezi kutukana watu kama kina
mama Karume, inaonekana klabu imemshinda kwani aliingia madarakani kwa
bahati tu na matokeo yake kaleta mgawanyiko badala ya umoja”,alisema
mzee Bilal Chakupewa.
Aidha
Mzee Chakupewa aliongeza kwamba hata kama wakiifunga Simba jumamosi
Nchunga ni lazima aondolewe madarakani kutokana na udhaifu aliouonyesha
kwenye uongozi wake na kuifikisha Yanga mahala pabaya
No comments:
Post a Comment