"Simjui huyo Ney ni nani
anaigiza filamu au ni demu gani? mimi najua majina kama hayo ni ya
mademu sasa iweje Neema anidiss mimi?"
NI
kauli ya nyota mwenye 'Crown' ya mkali wa Rhymes nchini Seleman
Msindi 'Afande Sele' alipokuwa akizungumza na Teentz.com kuhusiana na
'diss' dhidi yake iliyotolewa na msanii mwenye uwezo mkubwa wa kuchana
hivi sasa hapa Bongo, Ney wa Mitego kupitia track yake mpya iliyopewa
jina la 'Nasema Nao'.
Akizungumza
na mtandao huu namba moja ka habari za mastaa, Afande Sele mwenye
maskani yake pande za Morogoro amesema kuwa kamwe hajawahi kusikia
wala kujua kama kuna msanii wa hip hop hapa Bongo anayeitwa Ney na
kusisisitiza kuwa hamjui huyo mtu kabisa.
Alipotakiwa
kusema kama ameisikia Track hiyo Sele alifunguka kuwa hajui kitu
chochote kuhusu wimbo huo na anaamini kuwa hakuna wimbo wa Hip hop
ulitolewa hivi karibuni.
"Binafsi
sijaisikia na sijui lolote,nitajaribu kufuatilia,nitaitafuta track hiyo
niisikilize na kama atakuwa amefanya hivyo basi nitamlinganisha na mtu
anayemtukana Usain Bolt halafu akaanza kukimbia alisema Sele.
No comments:
Post a Comment