MWENYEKITI
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Mbeya Mjini John
Mwambigija, amesema hayuko tayari kwenda kuhojiwa na polisi kuhusu
tuhuma zinazomkabili za kutoa kauli za uchochezi kwenye mikutano ya
hadhara.
Kauli
zinazodaiwa kutolewa na Mwenyekiti huyo zilitolewa kwenye mikutano ya
wananchi wakati wa ziara ya viongozi wa CHADEMA katika Jimbo la Lupa
Wilayani Chunya kwenye opareshini ya Chadema ya Twanga kotekote (NATO).
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, aliwaambia waandishi wa
habari kwamba Mwenyekiti huyo anahitajika polisi kwa ajili ya kutoa
maelezo kuhusu tuhuma zinazomkabili.
Alisema,
moja ya tuhuma zilizolifikia jeshi la polisi kutoka kwa wananchi ni
kwamba kiongozi huyo amekuwa akitoa maneno ya uchochezi huku
akiwahamasisha wananchi kufanya vurugu zilizoambatana na uharibifu wa
mali za watu.
Alisema,
kiongozi huyo akiwa katika mikutano, wananchi hueleza matatizo
yanayowakabili amekuwa akiwahamisisha wakazi hao kudai haki kwa kufunga
barabara na hata kuchoma nyumba za viongozi kama walivyofanya uharibifu
wa mali za askari katika Kata ya Lupa Tinga-Tinga.“Kiongozi
huyu amekuwa akiwahamasisha wananchi kuchoma matairi ikiwa na kufunga
barabara pindi wanapotaka kutatuliwa madai yao kwa serikali jambo ambalo
ni kinyume cha utaratibu wa sheria, hivyo jeshi la polisi linamtaka
kiongozi huyo kufika kituoni ili kutoa maelezo ya tuhuma
zinazomkabili,”alisema.
Alisema,
kazi ya askari ni kupokea malalamiko kwa maandishi na kuyafanyia kazi
na kwamba katika utekelezaji askari huchukua maelezo ya pande zote mbili
na ndio maana kiongozi huyo anahitajika kwenda kutoa maelezo ya upande
wa pili.
Aidha,
Kwa upande wa Mwambigija alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari
mara baada ya kumaliza opareshini yao, alisema yeye yupo tayari kwenda
kituo cha polisi endapo atakuwa na makosa ya jinai lakini kwa masuala ya
kisiasa hawezi kufanya hivyo na endapo wataendelea kumfuatilia
patachimbika kupitia nguvu ya umma.
Alisema,
kazi ya jeshi la polisi ni kufanyia kazi taarifa wanazozitoa na si
kumwita yeye kwenda kutoa maelezo na kwamba wanachokifanya wao kwa
wananchi ni kutoa elimu jinsi ya kukabiliana na changamoto za maisha.
“Polisi
tunawasaidia kufanya kazi na mimi sitaenda polisi kwa sababu tu za
kisiasa kama ni hivyo CHADEMA kinawanasheria wengi ambapo tumekuwa
tukikamatwa mara kwa mara na tunashinda kesi hizo,”alisema
Mwambigija
na kuongeza kuwa chama cha CHADEMA kinanguvu ya umma isiyotumia silaha
bali maneno hivyo hatuwezi kufundishwa kutumia maneno matamu majukwaani.
Alisema,
kitendo cha polisi kuwaita kituoni kwa ajili ya kutoa maelezo eti kwa
sababu walitoa maneno makali na kwamba hilo ni jambo ambalo hawezi
kulifanya kamwe bali kama ingekuwa ni kosa la jinai.
Hivi
karibuni Mjumbe wa mkutano Mkuu Taifa kupitia chama cha Chadema, Edo
Mwamalala alilitupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kumchukulia
hatua Mwenyekiti huyo wa Chadema wilaya kutokana na kauli zake za
uchochezi anazozitoa kwenye mikutano ya hadhara
Mbeya yetu blog.
|
No comments:
Post a Comment