skip to main |
skip to sidebar
MTOTO WA AJABU MWENYE VICHWA VIWILI AZALIWA TANZANIA
Mwanamke mmoja amejifungua mtoto mwenye vichwa viwili katika hospitali teule ya Wilaya ya Bunda, mkoani Mara.
Mganga Mkuu wa hospitali ya DDH Bunda, Dk. Willam Krekamoo, amemtaja
mwanamke huyo kuwa ni Sarah Abenenego (16), mkazi wa mtaa wa Chiringe,
mjini Bunda.
Dk. Krekamoo alisema mwanamke huyo alipokelewa hosptilini hapo usiku wa
kuamkia jana akiwa anaumwa uchungu, na kwamba muda mfupi alijifungua
mtoto wa kike akiwa na vichwa viwili, midomo miwili, macho manne na
masikio manne.
Alisema mtoto huyo alizaliwa akiwa pia na mikono miwili na miguu miwili na kwamba baada ya muda mfupi alipoteza maisha.
Alisema uchunguzi unaonyesha kuwa ujauzito ulikuwa wa miezi saba na huo
ulikuwa ni uzazi wake wa kwanza na kuongeza kuwa hali ya mwanamke huyo
inaendelea vizuri.
No comments:
Post a Comment