Nape akihutubia baada ya kufungua kitega uchumi hiko, ambacho ni
milango ya maduka 37 pamoja na kituo cha mafuta"petrol station'' mali ya
CCM sumbawanga.
Kiongozi wa Kikundi cha Chipukizi wa Manispaa ya Sumbawanga Samira
Samir akimfunga skafu Katibu wa Itikadi na uenezi Taifa Ndugu Nape
Nnauye. Nape atakuwepo Sumbawanga kwa siku mbili katika ziara ya
kuimarisha Chama.
Chipukizi wa Chama cha Mapinduzi wa Manispaa ya Sumbawanga wakiwa
wamesimama kikakamavu wakisubiri kumpokea katibu wa Itikadi na Uenezi
ndugu Nape pamoja na Ujumbe wake wa watu Sita walio katika Ziara ya
kuimarisha Chama Mkoani Rukwa.
Katibu wa itikadi na Uenezi Taifa, Ndugu Nape Moses Nnauye akifungua
kituo Cha Uwekezaji na kitega Uchumi cha Chama Cha Mapinduzi (CCM)
katika maeneo ya Sabasaba, Manispaa ya Sumbawanga Mjini, Mkoani Rukwa
Leo Tarehe 14 july 2012.
Waziri wa Maji na Mbunge wa Mwanga Mhe. Jumanne Maghembe akisalimiana
na wakazi na viongozi wa Chama Mkoani Rukwa Ndugu Emanuel Seleman m-NEC
(katikati) pamoja na Mzee Abdillah(wa kwanza kulia) waliokuja kuwapokea
uwanja wa Ndege wa Sumbawanga mjini, Mhe. Maghembe ameongozana na Mhe
Nape Katika Ziara yake hiyo.
Nape akisalimiana na wenyeji wa Sumbawanga waliojitokeza uwanja wa
Ndege kumpokea. Katika Ziara yake hiyo Mheshimiwa Nape ameongozana na
Viogozi wa Chama na Serikali akiwemo Mhe. Mwigulu Nchemba(katibu wa NEC-
Uchumi na Fedha) Mhe. A. Mwanry (NW Tawala za Mikoa), Prof Jumanne
Maghembe, Mb (Waziri wa Maji), Mhe. Benedictor Ole Nangoro Naibu Waziri
wa Ujenzi., Dr Tizeba Charles (Mb,Nw Uchukuzi) Adam A. Malima(Naibu
Waziri Kilimo)
Bi Rahel Ndegeleke Katibu wa Mkoa wa Rukwa, Mwigulu Nchemba(Mb)
katibu wa NEC Uchumi na Fedha (katikati) na Nape Nnauye Katibu wa NEC
itikadi na Uenezi (kulia) mara baada ya kufika katika uwanja wa Ndege
wa manispaa ya Sumbawanga Mkoani Rukwa.
No comments:
Post a Comment