Gari
lenye namba za T 608 BWD lililokamatwa na kazi mbalimbali za wasanii
zikiwemo zinazosambazwa na Kampuni ya Steps ya jijini Dar es salaam
linalofanya kazi na wasanii hao
Moja ya gari lililokuwa limejaa kazi za wasanii
mbalimbali nchini zinazouzwa kiholera baada ya kurudufu kinyume na
sheria na kukosesha wasanii mapato mazuri.
BAADHI YA KAZI FEKI ZA WASANII ZILIZOKAMATWA LEO
MSANII MOHAMED
NICE 'MTUNISI' AKIZUNGUMZA JINSI WALIVYOKAMATA MZIGO FEKI WA KAZI ZA
WASANII MBALIMBALI KWA KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA STEPS ENTATAINMET YA
JIJINI DAR ES SALAAM INAYOSAMBAZA KAZI ZA WASANII NCHINI
MSANII MOHAMED
'NICE' AKILIA KWA UCHUNGU BAADA YA KUKUTA KAZI ZAO ZILIZOKUWA ZIKIUZWA
KATIKA MOJA YA DUKA MTAA WA MAGILA NA LIKOMA LEO
MTUUMIWA WA KURUDUFU KAZI ZA WASANII AKIWA CHINI YA ULINZI BAADA YA KUKAMATWA
WASANII
MZEE YUSUFU KUSHOTO NA MOHAMED NICE WAKIWA KATIKA DUKA LILILOKAMATWA
KWA KUUZA KAZI FEKI ZA WASANII MSAKO HUO ULIWASHILIKISHA KAMPUNI YA
STEPS ENTATAINMENT PAMOJA NA WASANII WENYEWE
MSANII
KAPTEN RADO AKIKAGUA KAZI ZAKE MPYA AMBAPO KAZI YAKE MPYA IJULIKANAYO
KAMA 'HATIHANI' ILIYOINGIA MTAANI LEO ILIKUWA IMESHA CHAKACHULIWA NA
KUINGIZWA SOKONI
Msanii
wa filamu nchini Mohamed Nice 'Mtunisi' kushoto na Jacob Stevin 'JB'
wakiwa katika duka ambalo lilikuwa linauza kazi zao ambazo ni feki
ambapo walikamatwa kwa kushilikiana na Kampuni ya usambazaji ya Steps
Entantainment ya jijini Dar es salaam
MSANII
MOHAMED NICE 'MTUNISI' KUSHOTO AKITOA MAELEZO MBALIMBALI KWA MAOFISA
USALAMA WALIOFIKA KATIKA UKAMATAJI WA KAZI FEKI ZA WASANII
Baazi ya wasanii pamoja na askari polis wakiwa wamerizingira duka lililokuwa linauza kazi za wasanii feki
BAADHI YA WANANCHI WAKISHUDIA TUKIO HILO
Baazi ya watu wakiwa wamezagaa kushudia ukamatwaji wa kazi za wasanii mtaa wa Magili na Likoma Dar es salaam leo
--
KAMPUNI ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam inayosambaza kazi
za wasanii kwa kushirikiana na wasanii wamekamata kazi mbalimbali za
wasanii hawo zinazorudifiwa kinyume na taratibu na kutofaidika kwa
wasanii wanaotoa kazi hizo
Msemaji wa Kampuni ya Steps Kambarage Ignatios amesema kuwa
ukamataji huo si wa zimamoto watahakikisha wanashilikiana na wasanii
wenyewe kukamata kazi zao mana wasanii wengi wanadai kuwa kazi zao
zinatoka sana kumbe zinachakachuliwa na kuwapa faida watu ambao wanakaa
tu na kusubili kazi za wasanii ameiomba serekali kuchukua atua kali ili
iwe fundisho kwa watu wanaorudufu na kunyonya kazi za wasanii hawo
Na mmoja ya wasanii waliojitokeza katika kamatakamata hiyo
iliyofanyika makutano ya mtaa wa Magila na Likoma Kariakoo, Msanii
Mohamedi Nice 'Mtunisi' amesema watu hawa wana akili za ziada kwani
katika kava ya mbele wanaweka stika yetu halali na dvd ndio inakuwa
imechakachuliwa akiangua kilio na kusema wasanii wakifa wanakufa
masikini kumbe ni watu wachache ndio wamekuwa wakinufaika na kazi zao
bila kushiriki chochote
Baadhi ya wasanii walioshiliki katika kamata kamata hiyo ni pamoja
na Jacobo Stevin 'JB' Mzee Yusuph wa kundi la Taarabu la Jahazi Simoni
Mwapagata (Rado) Mussa Msuba wa iliyokuwa Segere Orginal Seles
Mapunda ,Mohamed Nice 'Mtunisi' na wengine wengi wasanii hawo wameungana
pamoja kwa ajili ya kutetea kazi zao ili zisirudufiwe kiolela na
kuiomba serekali kupitisha sheria kali kwa mtu anaekamatwa na kazi kama
hizo zilizokamatwa
No comments:
Post a Comment