Henry Matata na Adam Chagulani
DIWANI wa Kata ya Kitangili Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza Henry Matata na Diwani wa
Kata ya Igoma Halmashauri ya Jiji la Mwanza (Nyamagana) Adam Chagulani
wote kutoka Chama cha CHADEMA wametoa tamko lao kwa vyombo vya habari
leo kupinga maamuzi ya Kamati kuu ya Chama hicho ya kuwavua uanachama
hivi karibuni kwa madai ya kukisaliti chama na kula njama kukushinikiza
kumung’oa aliyekuwa Meya wa Jiji la Mwanza Josephat Manyerere (Nyakato).
Diwani
Matata (Kitangili) alisema kwamba kikao cha kamati kuu kilichoketi
mwishoni mwa juma lililopita na kutoa uamuzi huo Jijini Dar es salaam
kiligubikwa na ushabiki na pia ukiukwaji wa Katiba ya Chama hicho na ile
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hivyo wameamua kwenda mahakamani
kufungua kesi ya kuzuia uamuzi huo wa Kamati kuu ya CHADEMA wa kuwavua
uanachama ili kukosa madaraka (Udiwani) ikiwa wao walichaguliwa na wananchi zaidi ya elfu nne.
Akifafanua
Matata amedai kuwa moja ya sababu kubwa zilizowafanya kukimbilia
mahakamani yeye na diwani mwenzake Chagulani ni kutaka haki itendeke kwa
vile madai na tuhuma zilizotolewa dhidi yake ni za uongo ambazo hazina
ukweli bali kwa shinikizo la wabunge wa chama hicho wa majimbo ya
Ilemela,Nyamagana na Ukerewe kutokana na kuwepo kutokuelewana baina yao
na madiwani hao wanaodaiwa kuwahofia kisiasa.
Kwa
upande wake Chagulani (Igoma) alieleza kuwa hatua hiyo imetokana na
Kamati kuu ya chama hicho Taifa kukubaliana na mapendekezo yaliyotolewa
na baadhi ya viongozi ambao wamekuwa akishirikiana na wabunge wa Chama
hicho wa Majimbo ya Ilemela Haghiness Kiwia na Ezekia Wenje Nyamagana
kutokana na wao kutofautiana nao kwenye vikao vya baraza la madiwani na
vya chama wakati wa kuchangia hoja kwa lengo la kuwatumikia wananchi
waliowachagua.
Chagulani
alisema kwamba umefika wakati wa viongozi wa chama hicho kuacha kutumia
ubabe wa kuamua kuwafukuza wawakirishi wa wananchi waliochaguliwa kwa
kisingizio cha kukisaliti chama hicho bali watambue kuwa wao ni kiungo
cha kuwatumikia wananchi na kuwawakilisha kwenye mabaraza ili
kuzitafutia kero zao ufumbuzi na CHADEMA lazima itumie vikao vya chini
na kuifuata vyema Katiba yake na hatua za wenye makosa kujadiliwa
kuanzia ngazi ya kata,wilaya,mkoa na Taifa badala ya kuanzia juu kasha
kutoa uamuzi hiyo si demokrasia hata kidogo bali ni udikiteta wa
demokrasia ndani ya vyama vya siasa.
No comments:
Post a Comment