Kamishna
wa Polisi Mussa Ali Mussa akifafanua jambo katika Mkutano na Waandishi
wa Habari akielezea juu ya Fujo na Ghasia zilizotokea katika Mkoa wa
Mjini Magharibi na kupelekea kifo cha Askari Mmoja,Mkutano huo
umefanyika hapo katika Makao Makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
Askari mmoja wa Jeshi la Polisi F.2105 Coplo Said Abdulrahaman wa Kikosi cha FFU Mkoa Mjini Magharibi ameuliwa kinyama kwa kupigwa mapanga kichwani na mikononi wakati akirudi kazini majira ya saa 6.30 usiku wa kuamkia leo katika eneo la Bububu.Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ziwani leo, Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa amesema mauaji hayo yamesababishwa na fujo za wafuasi wa Jumuiya ya UAMSHO baada ya kuenea uvumi wa kutekwa Msemaji Mkuu wa Jumuiya hiyo Sheikh Farid.
No comments:
Post a Comment