Cameroon
leo imebadunduliwa nje ya fainali za kuwania kombe la mataifa bingwa
barani Afrika zitakazo andaliwa nchini Afrika Kusini, licha ya kushinda
mechi yao ya raundi ya pili kwa mabao mawili kwa moja dhidi ya Cape
Verde hii leo mjini Yaunde.
Cape Verde iliilaza Cameroon kwa mabao mawili kwa bila katika mechi yao ya raundi ya kwanza.
Kabla ya
mechi hiyo Cameroon ilihitaji kuishina Cape Verde kwa zaidi ya magoli
mawili ili kujikatia tikiti ya kushiriki katika fainali hizo.
Cape
Verde ambayo imeorodhesha nyuma ya Cameroon katika orodha ya timu bora
ulimwenguni, imeandikisha historia kwa kufuzu kwa fainali hizo za
kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika kwa mara ya kwanza baada
ya kuishinda Indomitable Lions kwa jumla la magoli matatu mwa mawili.
Katika mechi nyingine ya kufuzu, Ethiopia ilivaana na Sudan ambapo Ethiopia imeibuka na ushini wa mabao mawili kwa bila.
Katika mechi ya raundi ya kwanza Sudan ilishindakwa mabao matano kwa matatu.
Ethiopia sasa imufuzu kupitia sheria ya goli la ugenini baada ya timu hizo kufungana jumla ya magoli matano kwa matano.
No comments:
Post a Comment