Rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, anapelekwa Ufaransa kwa matibabu zaidi baada ya kujeruhiwa alipopigwa risasi.
Wakuu
walisema rais alijeruhiwa wakati wanajeshi wa serikali waliokuwa kwenye
doria, walipofyatulia risasi msafara wa rais.Kabla ya kuondoka kuelekea
Paris, Rais Abdel Aziz alisema kwenye hotuba iliyotangazwa kwenye
televisheni kutoka hospitali, kwamba ameshafanyiwa upasuaji ambao
ulifanikiwa.
Inaarifiwa kuwa maafisa wawili wa jeshi wamekamatwa.
Jenerali
Abdel Aziz, ambaye anaonekana na mataifa ya magharibi kuwa anasimama
dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu katika eneo hilo, alichaguliwa mwaka wa
2009, mwaka mmoja baada ya kupindua serikali
No comments:
Post a Comment