Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, October 14, 2012

Kaskazini Unguja Watoa Maoni Katiba Mpya



 Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (aliyesimama) akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja wakati wa mkutano
ulioitishwa jana tarehe 13 Oktoba, 2012 na Tume hiyo kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba
kijijini hapo. Wengine pichani (kutoka kulia) ni Wajumbe wa Tume hiyo, Joseph Butiku (kulia), Profesa
Paramagamba Kabudi, Katibu wa Tume, Assaa Rashid na Naibu Katibu Casmir Kyuki.

 Wananchi wa Kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja, Zanzibar
wakifuatilia kwa makini mkutano ulioitishwa jana tarehe 13. Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya
Katiba kijijini hapo wenye malengo ya kukusanya maoni yao kuhusu mchakato wa Mabadiliko ya Katiba.
  Bw. Yusuph Juma (60) mkazi wa Kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini Unguja,
Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa jana tarehe 13.
OOktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.
 Bw. Said Haji Makame (21), mkazi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini
Unguja, Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa jana tarehe 13.
Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo.
Bi. Tatu Maalim Mganga (65) mkazi wa kijiji cha Kidombo Wilaya ya Kaskazini A Mkoa wa Kaskazini
Unguja, Zanzibar akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano ulioitishwa jana tarehe 13
Oktoba, 2012 na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo

No comments:

Post a Comment