Mkuu wa
wilaya ya Singida mwalimu Queen Mlozi akitoa taarifa kwa waandishi wa
habari (hawapo kwenye picha) juu ya ujio wa tume ya kukusanya maoni ya
Katiba kwenye wilaya hiyo.
(Picha na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Tume ya
mabadiliko ya katiba, inatarajia kuanza kukusanya maoni ya wananchi wa
wilaya ya Singida kuanzia oktoba 17 hadi 27 mwaka huu.
Akitoa
taarifa ya ujio wa tume hiyo wilayani humo kwa waandishi wa habari hiyo
Mkuu wa wilaya ya Singida Mwalimu Queen Mlozi amesema wilaya hiyo
yenye halmashauri mbili, tume hiyo itaanza kukusanya maoni kwenye kata
kumi za halmashauri ya manispaa ya Singida kuanzia Oktoba 17 hadi 21
mwaka huu.
Amezitaja kata hizo za manispaa kuwa ni wankoko,Unyambwa,Mandewa,Mtipa,Kisaki,Mungumaji,Majengo,Unyambwa,Mughanga na Mtamaa.
Aidha,
mkuu wa wilaya amesema kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya Singida
vijijini, tume hiyo itaanza kukusanya maoni kuanzia oktoba 22 hadi 27
mwaka huu.
Mlozi
ametaja kata zilizochaguliwa kutembelewa na tume hiyo kuwa ni
Msisi,Kinyeto,Mtinko,Maghojoa,Mgori,Ngimu,Merya,Ilongero,Maghojoa,Mgori,Ngimu,Merya,Ilongero,
Ughandi na Ngamu.
Amesema
kila siku tume hiyo itakapo tembelea kata mbili ambapo kata ya kwanza
wananchi watatoa maoni yao kuanzia saa tatu asubuhi na kata ya pili
shughuli itaanza saa nane mchana.
Alitumia
fursa hiyo kutoa wito kwamba wananchi wajitokeze kwa wingi kutoa maoni
yao wakati watakapokuwa wanapewa muda wa dakika tano na endapo
itashindikana kutumia njia hiyo,basi watumie njia ya kuandika maoni yao
kwa maandishi.
Pia amewaonya kwamba wasishawishiwe na mtu au kiongozi katika kutoa maoni yao.
No comments:
Post a Comment