13th
November 2012
Bei za
vyakula katika masoko ya jijini Dar es Salaam zimeendelea kuwa juu, huku soko
la Kisutu likionekana kuwa kinara wa kuuza bidhaa kwa bei ya juu ukilinganisha
na masoko mengine.
Uchunguzi
uliofanywa na NIPASHE jana umebaini kuwa bei za vyakula katika masoko hayo
zimekuwa zikipanda kwa kasi kubwa kiasi cha kuzidisha makali ya maisha kwa
wakazi wa jiji hilo.
Kinachoshangaza
ni kwamba, hata Soko Kuu la Kariakoo, ambalo hapo zamani lilikuwa ni kimbilio
la wengi, hivi sasa bei zake ni kali mno.
Hali ni
kama hiyo pia kwa masoko ya Temeke, Magomeni, Tandale na Mwanamyamala.
Hata
hivyo, bei za bidhaa zinazouzwa katika masoko hayo zimekuwa tofauti
zikilinganishwa na zile za katika soko la Kisutu lililopo katikati ya jiji.

No comments:
Post a Comment