Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 13, 2012

MSIBA KWENYE MZIKI WA TAARABU::::MARIAM KHAMIS(PAKA MAPEPE)AFARIKI DUNIA

 
 
 Msanii wa taarab nchini Tanzania wa kundi la TOT plus, Mariam Khamis maarufu kama paka mapepe amefariki dunia usiku wa jana kuamkia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam mara tu baada ya kujifungua .

Mariam Khamis umauti umemkumba akiwa anaimba kundi la TOT plus lakini enzi za uhai wake aliwahi kuimbia katika makundi mbalimbali ya taarab likiwemo East Africa Melody, Zanzibar Stars na 5 Stars.

Khamis Muhidini Shomary baba wa marehemu amesema mipango ya mazishi inaendelea kufanyika ambapo anatarajiwa kuzikwa hapo kesho Magomeni Kota jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment