Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Tuesday, November 20, 2012

Tume Ya Mabadiliko Ya Katiba Yaanza Kukusanya Maoni Ya Wananchi Wilaya Ya Karatu Arusha



1.   Mkuu wa Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Daudi Ntibenda akizungumza na wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba (hawapo pichani) jana jumatatu Novemba 19, 2012 wakati wajumbe hao walipofika ofisini hapo kabla ya kuanza kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya Wilayani humo. Kushoto ni mjumbe wa Tume, Bi. Mwantumu Malale.

Akina Mama wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha wakisoma nakala za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Sheria ya Mabadiliko ya Katiba katika lugha nyepesi wakati wa mkutano wa kazi ya ukusanyaji wa maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya ulioitishwa na Tume  ya Mabadiliko ya Katiba kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012
1. Mjumbe wa Sekretarieti ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Charles Masero (mwenye shati jeupe) akitoa ufafanuzi kuhusu ujazaji wa fomu za maoni kuhusu Katiba Mpya kwa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi cha Audry Veldan kilichopo kijiji cha Shahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ya maoni ya wananchi kuhusu Katiba Mpya kijijini hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012.

  Mkazi wa kijiji cha Slahhamo Kata ya Mbulumbulu Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Thimos Mushi (51) akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya wakati wa mkutano wa kukusanya maoni ulioitishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba kijiji hapo jana jumatatu Novemba 19, 2012.
Mkazi wa Kata ya Rhotia Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, John Nando (73)akitoa maoni yake kuhusu Katiba Mpya mbele ya Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba wakati wa mkutano ulioitishwa na Tume hiyo jana jumatatu Novemba 19, 2012 katika Kata hiyo.

No comments:

Post a Comment