| Sehemu ya ukuta uliobomoka |
Sehemu ya ukuta iliyobomoko na kusababishaa kifo cha mwanafunzi mmoja
| Wasamaria wema wakijaribu kumwokoa kijana aliyeangukiwa na ukuta kwa kufukua kifusi kwa mikono |
Mwanafunzi
wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Kwakilosa katika
Manispaa ya Iringa Daniel Yona (15) amefariki dunia baada ya
kuaungukiwa na ukuta wa uwanja wa Samora wakati akijaribu kupita
mlango wa panya ili kwenda kushuhudia tamasha hilo la Mtikisiko
2012.
Tukio
hilo lilitokea usiku wa kuamkia Desemba 2 mwaka huu wakati wapenda
burudani katika mkoa wa Iringa walipofika katika uwanja huo kushuhudia
onyesho kubwa la Mtikisiko 2012 ambalo lilikuwa limepambwa na wasanii
mbali mbali wakiongozwa na mkongwe Juma Nature na Profesa J.
Wakielezea
kilichomkuta mwanafunzi huyo baada ya mashuhuda walisema kuwa
mwanafunzi huyo na wenzake waliacha kupita katika mlango wa kawaida
kwa kulipia kiingilio halali kilichowekwa na badala yake aliamua
kupita gizani na kupanda ukuta huo wa uwanja wa Samora ili kuweza
kuingia ndani ya uwanja huo kuona tamasha la Mtikisiko.
Hata
hivyo mmoja kati ya mashuhuda ambae hakupenda kutajwa jina lake hapa
alisema kuwa kabla ya mwanafunzi huyo kupanda ukuta huo kuna vijana
kama 20 ambao walifanikiwa kupita eneo hilo bila kulipa kiingilio
na baada ya kufanikiwa kupita walianza kupigiana simu huku baadhi
ya vijana wa kitanzini wakiwatoza vijana hao wanaoruka ukuta
kiingilia cha shilingi 1000 hadi shilingi 500 .
"Ujue
hapa vijana wa kihuni kutoka Kitanzini walikuwa wamejipanga hapa na
kufanya ufisadi wa kuwatoza watu kiingilio bila wahusika wa Tamasha
hilo kujua kinachoendelea .....hivyo hata huyo mwanafunzi alikuwa ni
mmoja kati ya wavamizi wa Tamasha hilo kwa kupita njia ya panya
ili kuingia ndani ya uwanja huo"
Pia
alisema ukuta huo ulionyesha kuzidiwa nguvu kutokana na ubovu wa
ukuta wenyewe kuwa ni mbovu na ulikuwa umeungwa kienyeji katika eneo
hilo .
Aidha
alisema baada ya vijana zaidi ya watano kupanda eneo hilo la ukuta
ambalo lipo upande wa kushoto mwa uwanja huo wa uwanja ukuta huo
ulionyesha kuyumba na kupelekea vijana wengine kuruka na kumwacha
mwanafunzi huyo ambae tayari alikuwa ameingiza mguu mmoja ndani ya
uwanja na mguu wa pili ulikuwa nje.
Alisema
baada ya ukuta huo kuanguka na kumfunika walifanikiwa kumwokoa akiwa
hai na kumkimbiza Hospitali ya mkoa wa Iringa ambako asubuhi ya siku
ya pili ya Desemba 2 majira ya saa 5 asubuhi alifariki dunia.
Hata
hivyo askari polisi waliokuwepo eneo hilo la tukio walimthibitishia
mwandishi wa mtandao huu kuwa ni kweli kijana huyo amefariki dunia
japo wao si wasemaji wa jeshi la polisi na kudai kuwa chanzo ni
kijana huyo mwenyewe kutaka kupita mlango wa panya na kuacha kupita
mlangoni ambako watu wote walikuwa wakipita bila kupata matatizo
yoyote.
Hata
hivyo uchunguzi wa mtandao huu unaonyesha kuwa kifo cha mwanafunzi
huyo kimesababishwa na mwanafunzi mwenyewe kutokana na kutaka kupita
njia ya panya na kuacha mlango kwani iwapo angetumia njia sahihi
kuingia uwanjani yawezekana kifo kisingeweza kutokea .
Source: Francis Godwin Blog

No comments:
Post a Comment