Wachezaji wa Tusker wakimpongeza mfungaji wa bao lao, Ismail Dunga kulia |
MABINGWA
wa Kenya, Tusker FC jioni hii wameiangusha Yanga SC bao 1-0 kwenye
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kirafiki jioni hii.
Huo
ulikuwa mchezo maalum kwa Yanga kuwaaga mashabiki wake, kabla ya safari
ya Uturuki Jumamosi usiku kwenda kuweka kambi ya wiki mbili.
Hadi
mapumziko, Tusker walikuwa tayari mbele kwa bao hilo 1-0, lililowekwa
kimiani na kiungo Ismail Dunga kwa mkwaju wa penalti dakika ya 44.
Refa
Charles Oden Mbaga alitoa penalti hiyo baada ya kiungo wa Yanga, Nurdin
Bakari kumuangusha kwenye eneo la hatari, kiungo Khalid Aucho.
Yanga
walicheza vema katika kipindi hicho, lakini hawakufanikiwa kutengeneza
nafasi za kufunga na hilo lilitokana na mipango haba ya safu yake ya
kiungo leo, ikiongozwa na Kabange Twite na Nurdin Bakari.
Pamoja
na kocha Mholanzi Ernie Brandts kufanya mabadiliko kipindi cha pili,
akiwaingiza Hamisi Kiiza, Jery Tegete, Simon Msuva, Omega Seme na Nizar
Khalfan kuchukuwa nafasi za akina David Luhende, Said Bahanuzi, George
Banda, Rehani Kibingu na Oscar Joshua, lakini matokeo hayakubadilika.
Zaidi
Yanga iliongeza kasi ya mashambulizi kupitia kwa Msuva na Kiiza na hata
Nizar alipoingia, lakini kwa ujumla bahati haikuwa yao jioni ya leo.
Hii
ni mechi ya pili Brandts anafungwa kati ya mechi 10 alizoiongoza Yanga
tangu aanze kazi akirithi mikoba ya Mbelgiji, Tom Saintfiet, nyingine
saba ameshinda na moja ametoa sare.
Yanga
SC; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Nadir Haroub
‘Cannavaro’, Ladislaus Mbogo, Nurdin Bakari, Rehani Kibingu, Kabange
Twite, George Banda, Said Bahanuzi na David Luhende.
Tusker
FC; George Opiyo, Luke Ochieng, Jeremiah Bright, Mark Odhiambo, Joseph
Shikokoti, Khalid Aucho, Edwin Manono, Justin Monda, Ismail Dunga, Jesse
Were, Robert Omonuk,
No comments:
Post a Comment