Wachezaji wa Young Africans wakiwa mazoezin leo asubuhi katika viwanja vya Fame Residence football |
Kikosi
cha Young Africans leo asubuhi kimeendelea na mazoezi katika viwanja
vya Fame Residence baada ya jana kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya
timu ya Arminia Bielefeld ambao uliishia kwa sare ya bao 1-1 mchezo
uliofanyika katika uwanja wa Adora football Belek - Antalya.
Kocha
Brandts ameendelea kukifua kikosi chake na kufanyia marekebisho ya
baadhi ya makosa yaliyojitokeza katika mchezo wa jana ambao hata hivyo
Yanga iliutawala kwa kipindi chote cha mchezo.
Arminia
Bielefeld ambao awali hawakutegemea Tanzania kuwa kunaweza kuwa na timu
ambayo inaweza kuwapa upinzania, walikiri mwishoni mwa mchezo kwamba
Yanga ina timu nzuri na hawak.utegemea kuona kiwango kizuri cha mchezo
kilichoonyeshwa na vijana na wa Jangwnai alisema mmoja wa maofisa wa
Arminia Bielefeld.
Ukizingatia
Armini Bielefeld ilikuwa imetoka kuifunga Bayern Levekursen 4-2 katika
mchezo wa kombe la Ujerumani, walikutana na vijana wa Jangwani ambao
waliweza kuutawala mchezo huo kuanzia kwa mlinda mlango Ally Mustafa
'barthez, mpaka kwa washambuliaji wake.
Nahodha wa Young Africans Nadir Haroub 'Cannavaro' kushoto akisalimiana na wamuzi wa mchezo na nahodha wa timu ya Arminie Bielefeld kabla ya mchezo huo jana |
Brandts
alisema amefarijika na matokeo ya mchezo huo, japokuwa lengo lake kubwa
lilikuwa ni kupata ushindi katika mchezo huo lakini wachezaji wake
waliweza kufanya kazi nzuri sana uwanjani kitu kilichofanya Wajerumani
kushangaa.
Young
Africans mara baada ya mazoezi ya leo asubuhi, jioni itakua ikifanya
mazoezi ya kujenga mwili misuli (GYM) katika Hotel ya Fame Residence
Lara & Spa ambao kesho asubuhi itaendelea na mazoezi katika viwanja
vya Fame Residence
PICHA na habari kutoka mtandao wa yanga
No comments:
Post a Comment